Kwa picha: Mahujaji wa kigeni waruhusiwa kuingia Mecca kwa ibada ya Umrah
Mahujaji wa nchi za nje wameruhusiwa kufika kwenye msikiti mkuu mjini Mecca kwa mara ya kwanza tangu kuanza kutekelezwa kwa masharti ya kukabiliana na corona miezi saba iliyopita.

Chanzo cha picha, Reuters
Kuanzia leo Jumapili, baadhi ya mahujaji 10,000 kutoka nje ya nchi wameruhusiwa kufanya ibada ya Hija ya Umrah ambayo waislamu huweza kuitekeleza kipindi chochote kile.

Chanzo cha picha, Reuters
Mahujaji hao walilazimika kujitenga kwa siku tatu baada ya kuwasili Saudi Arabia kabla ya kuruhusiwa kuzunguka Kaaba - eneo takatifu zaidi katika dini ya Kiislamu - katikati ya msikiti mkubwa.

Chanzo cha picha, Reuters
Saudi Arabia imeripoti maambukizi 347,282 ya ugonjwa wa Covid-19 huku ikirekodi vifo 5,402 tangu kuanza kwa janga la virusi vya corona ilihali watu 333,842 wakithibitishwa kupona.
Nchi hiyo imeanza kufungua baadhi ya misikiti kama sehemu ya kulegeza masharti kote nchini humo.

Chanzo cha picha, Reuters
Wakaazi wa Saudi Arabia waliruhusiwa kufanya ibada ya Umrah Oktoba na idadi hiyo inazidi kuongezwa ili kuwezesha mahujaji wengi mwezi huu.

Chanzo cha picha, Reuters
Ni wakazi 10,000 Waislamu wa Saudia walioruhusiwa kufanya ibada ya kwenda kuhiji mwezi Julai mwaka huu, tofauti na mamilioni ya watu ambao wamekuwa wakishiriki ibada hiyo miaka ya nyuma, kama ilivyokuwa mwaka 2016 kwnye picha inayofuata.

Chanzo cha picha, EPA








