Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Robert Levinson: Iran yaamriwa kulipa dola bilioni 1 kwa familia ya Mmarekani aliyepotea
Jaji wa nchini Marekani ameamuru Iran ilipe $ 1.45bn pauni bilioni 1.12 kwa familia ya wakala wa zamani wa FBI ambaye alitoweka wakati wa ziara nchini humo mwaka 2007.
Uamuzi ulimpa mke wa Robert Levinson na watoto wake kiasi cha dola bilioni 1.35 kwa uharibifu na dola za Marekani milioni 107 fidia ya athari za utekaji nyara.
Hakukuwa na jibu la haraka kutoka kwa serikali ya Iran, ambayo imekuwa ikikanusha kila wakati kuwa haifahamu yeye ni nani na mahali alipo
Mamlaka za Marekani na familia ya Bwana Levinson wanaamini alikufa akiwa ameshikiliwa Iran.
Katika taarifa, walielezea uamuzi huo Alhamisi iliyopita uliofanywa na Jaji Timothy Kelly wa Mahakama ya huko Washington kama "hatua ya kwanza katika kutafuta haki".
"Hadi sasa, Iran haijalipa chochote kutokana na vitendo vyake," waliongeza.
"Uamuzi wa Jaji Kelly hautamleta Bob nyumbani, lakini tunatumaini kuwa itakuwa onyo dhidi ya Iran na vitendo vyake vya utekaji Iran."
Bwana Levinson alipotea wakati wa safari ya kisiwa cha Kish cha Iran katika eneo la Ghuba mnamo mwezi Machi mwaka 2007.
Serikali ya Marekani inasema Bwana Levinson alikuwa akifanya kazi huko kama mchunguzi wa binafsi kwa niaba ya mashirika kadhaa makubwa.
Lakini, vyombo vya habari vya Marekani viliripoti kwamba alikuwa kwenye misheni isiyoidhinishwa kwa ajili ya shirika la upelelezi la CIA, na kwamba akiwa Kish alikutana na mkimbizi wa Marekani Dawud Salahuddin.
Anasema Bw Levinson alimwambia kwamba alikuwa akichunguza usafirishaji haramu wa sigara katika Ghuba, na kwamba baada ya kukutana walikamatwa na vikosi vya usalama vya Iran.
Mnamo mwaka wa 2011, picha zilitumwa kwa familia ya Bwana Levinson ikimuonesha akiwa amevalia suti ya machungwa. Waziri wa mambo ya nje wa Marekani wakati huo, Hillary Clinton alisema aliamini kuwa alikuwa akishikiliwa "mahali fulani Kusini Magharibi mwa Asia".
Mke wa Bwana Levinson, Christine, aliiambia kamati ya bunge la Marekani mnamo Machi 2019 kwamba "ameachwa nyuma, amekuwa si kipaumbele, au anaonekana amesahauliwa" na Serikali ya Marekani zilizofuata.
Mapema mwaka huu, Mkurugenzi wa shirika la upelelezi FBI Christopher Wray aliiambia familia ya Bwana Levinson kwamba "ushahidi wa kuaminika zaidi ambao tumekusanya kwa miaka 13 iliyopita unaonesha uwezekano kwamba Bob alikufa akiwa kifungoni". Lakini alisisitiza kwamba FBI haikukata tamaa kupeleleza kilichotokea.
Wakati huo, Iran ilirudia kauli yake ya hapo kuhusu kesi hiyo, ikisema ilikuwa ikijaribu kujua hali ya Bw Levinson "lakini haikuweza kupata dalili zozote za yeye kuwa hai".
Katika uamuzi wake, Jaji Kelly alisema: "Mwenendo wa Iran hapa ni ... wa kipekee, ikizingatiwa kuwa - katika hali ya kushangaza - ilimnyakua wakala maalum wa zamani wa FBI na DEA bila tahadhari, ikamtesa, ikamshikilia kwa muda mrefu kama miaka 13, na hadi leo inakataa kuwajibika. "
"Na mkewe na watoto, na wenzi wao na watoto - wakati wanaweka kumbukumbu ya Levinson hai - imebidi waendelee na maisha yao bila kujua hatima yake hasa. Hakika haya ni matendo yanayostahili kukemewa kwa kiasi kikubwa," aliongeza.