Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Nyaraka zaFinCEN: Mwandani Putin aliyewekewa vikwazo ‘alitakatisha mamilioni ya fedha ’ kupitia benki ya Barclays
Mmoja wa marafiki wa Vladimir Putin huenda alitumia benki ya Barclays jijini London kutakatisha fedha na kukweba vikwazo, zimeonesha nyaraka zilizoonekana bila kukusudiwa.
Billionaire Arkady Rotenberg anafahamiana na rais wa Urusi tangu utotoni.
masharti ya kifedha , au vikwazo, viliwekwa dhidi ya Bw. Rotenberg Marekani pamoja na Muungano wa Ulaya mwaka 2014, ikimaanisha kuwa benki za magharibi zinaweza kukabiliwa na athari mbaya kwa kufanya nae biashara.
Barclays inasema kuwa ilititekeleza majukumu ya sheria na udhibiti.
Kupatikana kwa nyaraka za siri - "ripoti zinazoshukiwa" za benki - kunafichua jinsi kampuni zinazoaminiwa kuruhusiwa kudhibitiwa na Bwana Rotenberg zililivyotunza akaunti za siri.
Kipindi cha BBC panorama kimeshuhudia Nyaraka hizo , zinazofahamika kama FinCEN Files,
Wandani
Mwezi Machi mwaka 2014 Marekani iliiwekea vikwazo vya kiuchuchumi Urusi kufuatia hatua yake ya kulitwaa jimbo la Crimea nchini Ukraine.
Wizara ya fedha ilimuwekea vikwazo Bwana Rotenberg, 68, na kaka yake Boris, 63, " wandani wa uongozi wa Urusi ".
Wawili hao wamepata mafunzo mazoezi ya viungo ya Judo sawa na Putin wakati walipokuwa wadogo.
Katika miaka ya hivi karibuni , kampuni ya Arkady Rotenberg ilijenga barabra, bomba la gesi na kituo cha nishati kupitia mikataba aliyopewa na taifa la urusi.
Wizara ya fedha ilisema makaka hao "walisaidia miradi midogo ya Putin " na "kutengeneza mabilioni ya dola katika mikataba ya Gazprom na ule wa Olympiki ya majira ya baridi iliyotolewa kwao na Putin".
Mnamo mwaka 2018, Marekani iliongeza jina la mtoto wa Arkady Rotenberg, Igor kwenye orodha ya watu bnafsi waliowekewa vikwazo.
Lengo la vikwazo lilikuwa ni kuondoa watu waliotajwa kabisa kwenye mfumo mzima wa fedha wa magharibi.
Lakini bado Rotenbergs anaonekana kuendelea kutembeza fedha kupitia Uingereza na Marekani.
Mpango na utakatishaji wa pesa
Mwaka 2008, Barclays ilifungua akaunti ya benki ya akaunti ya kampuni inayoitwa Advantage Alliance.
Nyaraka zilizofichuliwa zinaonesha kampuni ikihamisha pauni milioni 60 kati ya mwaka 2012 na 2016. Uhamishaji mwingi wa pesa ulitokea bada ya makaka wa Rotenberg kuwekewa vikwazo.
Mwezi Julai , uchunguzi uliofanywa na Seneti ya Marekani uliwashutumu makaka wa Rotenberg kwa kutumia njama za siri kukiuka vikwazo-moja ya makampuni ilihusika katika mpango wa Advantage Alliance.
Wapelelezi wa marekani walisema kuwa kulikuwa na ushahidi mkubwa kwamba Advantage Alliance ulikuwa unamilikiwa na Arkady Rotenberg, na kwamba kampuni hiyo ilikuwa inatumia kaunti yake ya benki ya Barclays mjini kununua mamilioni ya sanaa kwa ajili yake.
Ripoti hiyo ilibaini "usiri, kutotambulikana, ukosefu wa taratibu za kubuni mazingira ya kumariza utakatishaji wa fedha na ukwepaji wa vikwazo". Minada wa nyumba Marekani na Uingereza "ilishindwa kuuliza maswali ya kimsingi " kuhusu wanunuzi wa sanaa.
Licha ya vikwa, Arkady wanaonekana kulipa dola milioni $7.5 walizopata kutokana na mchoro René Magritte La Poitrine.
Tarehe 17 Juni 2014 kampuni yenye uhusiano na Arkady ilituma fedha taslimu kutoka Moscow kwenye akaunti ya Alliance ya Barclays mjini London. Siku iliyofuatia Barclays ilituma fedha hizo kwa muuzaji wa mchoro huo mjini New York.
Kufungwa kwa akaunti
Mwezi Aprili 2016, Barclays ilianza uchunguzi wa ndani wa akaunti nyingi ambazo ilizishuku kuwa na uhusiano na makaka wa Rotenberg.
Miezi sita baadaye, benki hiyo ilifunga akaunti ya Advantage baada ya kuwa na hofu kuwa ilikuwa inatumiwa kusafirisha fedha zilizoshukiwa.
Lakini ripoti ya taarifa zilizoshukiwa ambazo zilizobainika kimakosa (SARs) inaonesha kwamba akaunti nyingine za Barclays zinazoshukiwa kuhusiana na makaka wa Rotenbergs ziliendelea kufunguliwa hadi 2017.
Moja ya kambuni za aina hiyo ilikuwa ni ile ya Ayrton Development Limited.
Kwamujibu wa nyaraka hizo, Barclays ilishuku shughuli za akaunti ya Ayrton na kusema kuwa "[Arkady] Rotenberg ni mmiliki halisi wa is akaunti Ayrton".
Barclays haikutoa kauli yoyote ilipoulizwa na BBC Panorama kuhusu jinsi akaunti nyingi ilizozishuku zilikuwa zinamilikiwa na Rotenbergs.
Msemaji wa Barclays alisema: "Tunaamini kwamba tumefuata sheria zote na masharti ikiwa ni pamoja na vikwazo vya Marekani ."
" Kuwasilishwa kwa suala la SAR pekee sio ushahidi wa kosa halisi, tungevunja tu uhusiano na mteja wetu baada ya uchunguzi makini na wenye lengo na tathmini ya ushahidi, kwa kuweka kwenye mizani uwezekano wa uhalifu wa kifedha unaoshukiwa na hatari ya 'kuondoa uanachama wa mteja ' kwa mteja asiye na hatia ."
Rotenbergs walikataa kutoa kauli yoyote.
Faili za FinCen ni taarifa ya BBC kinachoelezea kuvuja kwa nyaraka za siri ambazo zilifichua benki kuu zilzoruhusu pesa chafu kote duniani. Pia kinaonesha kuwa mara kwa mara Uingereza imekua kiunganishi dhaifu katika mifumo ya fedha ya kimataifa na jinsi London ilivyo na pesa za Urusi.
Faili hizo zilichukuliwa na mtandao wa BuzzFeed News ambao ulizishilikisha na Muungano wa waandishi wa habari wa kimataifa wa taarifa za uchunguzi (ICIJ) ana waandishi wa habari 400 kutoka maeneo mbalimbali duniani. Panorama iliongoza utafiti kwa ajili ya BBC.