Mabadiliko ya dunia yaliyosababisha Dinosaria kutawala dunia.

Milipuko mikubwa ya volkano iliyotokea miaka milioni 233 iliyopita ilitoa hewa ya ukaa, methane na mvuke wa maji hewani.

Utafiti wetu mpya umebaini kuwa hii ilikuwa tukio la lililowaua wanyama wengi aina ya tetrapod, na kutoweka kwa wanyama aina ya dinosaria.

Kutoweka huko kwa viumbe hao kulitokea mwishoni mwa kipindi cha cha kijiolojia kiitwacho kitaalamu Cretaceous, miaka milioni 66 iliyopita. Hapo ndipo dinosaria, pterosaria, wanyama watambaao wa baharini, na amoniti walipotea.

Tukio hili lilisababishwa na athari za asteroidi kubwa ambayo ilizima mwanga wa jua na kusababisha giza na kuganda, ikifuatiwa na mvurugiko kwenye bahari na hewa.

Wanajiolojia na Paleontolojojia wanakubaliana kuwa kulikuwa na matukio matano ya namna hiyo, ambayo kipindi cha Cretaceous ndio kilikuwa cha mwisho. Hivyo, ugunduzi wetu wa kupotea kwa viumbe kwa kiasi kikubwa huenda hakikuwa kimetarajiwa

Na bado tukio hili, lililopewa jina la Kipindi cha Carnian Pluvial, inaonekana kimeua spishi nyingi kama vile asteroid kubwa ilivyofanya. Mifumo ya ikolojia ya baharini na baharini ilibadilika sana wakati sayari ilipopata moto na kukauka.

Ardhini, hali hii ilisababisha mabadiliko makubwa kwenye mimea na wanyama wanaokula mimea. Kupungua kwa wanyama wanaokula mimea kama rhinosaurs na dicynodonts, kwa dinosaria iliikuwa ndio nafasi yao.

Dinosaria walitokea miaka milioni 15 mapema na utafiti wetu mpya unaonesha kuwa ni matokeo ya Kipindi cha Carnian Pluvial, waliongezeka haraka zaidi ya miaka milioni 10 hadi 15 na kuwa spishi kubwa katika mazingira ya ulimwengu.

Kipindi hiki kilisababisha "umri wa dinosaria kufikia miaka milioni 165.

Si tu dinosaria tu makundi mengine ya wanyama kama kobe, mijusi,mamba, na jamii ya mamali

Kwanza, wanajiolojia kutoka Ujerumani, Uswizi, na Italia walitambua mabadiliko makubwa katika wanyama wa baharini ambayo yalitokea miaka milioni 232 iliyopita, inayoitwa tukio la Rheingraben.

Kisha, mnamo 1986, nilitambua kuwa huku ni kubadilishana kati ya tetrapods na ammonites. Lakini wakati huo, mbinu za kuchangamana zilikuwa dhaifu sana kuliko sasa na haikuwezekana kuwa na uhakika ikiwa zote zilikuwa tukio moja.

Mafumbo yalianza kufumbuliwa wakati wanajiolojia Mike Simms na Alastair Ruffell walipotambua kote Uingereza na sehemu za Ulaya zenye hali ya hewa ya unyevu.

Baadaye, mtaalam wa jiolojia Jacopo dal Corso aligundua kwa bahati kwa wakati huo huo kati ya Kipindi cha Carnian Pluvial na kilele cha milipuko kutoka kwa mawe ya Wrangellia.

Wrangellia ni jina ambalo lilitolewa na wataalamu wa jiolojia kwa visahani vyembamba vinavyotengeneza uso wa dunia vilivyojishikiza kwenye eneo la pwani ya Magharibi ya bara la Amerika Kaskazini, Kaskazini mwa Vancouver na Seattle.

Mwishowe, katika kutathimini ushahidi wa mwamba wa Triassic,Kipindi cha Carnian Pluvial kiligunduliwa, sio Ulaya tu, bali pia Amerika Kusini, Amerika ya Kaskazini, Australia na Asia.

Milipuko mikubwa ya Wrangellia ilisababisha kutolewa kwa hewa ya ukaa, methane, na mvuke kwenye hewa, na kusababisha ongezeko la joto duniani na ongezeko la mvua duniani.

Kulikuwa na milipuko mpaka mitano iliyoambatana na joto kali tangu miaka 233 iliyopita

Milipuko hiyo ilisababisha mvua ya acid na gesi ya volkano ikichanganyika na maji ya mvua,bahari nazo hupatwa na acid.

Joto kali lilifanya wanyama wakimbie na mvua yenye acid iliua mimea ardhini, huku baharini nako viumbe vilishambuliwa na chembechembe zitokanazo na mvua hiyo.

Hii iliondoa uso wa bahari na ardhi. Maisha yalikuwa yameanza kurejea kama kawaida, lakini milipuko ilipokoma, joto lilibaki kuwa juu wakati mvua za kitropiki zilipoacha kunyesha.

Hali hii ilisababisha kukauka kwa ardhi ambayo dinosaria walikuwa wananufaika nayo.

Mabadiliko haya makubwa katika mizunguko ya kemikali baharini iliashiria mwanzo wa mfumo wa kisasa wa ikolojia ya baharini.

Kutakuwa na funzo muhimu kuhusu namna ya kuisaidia dunia baada ya hali ya mabadiliko ya tabia nchi.

Wanajiolojia lazima wachunguze kwa kina kuwa ni kwa namna gani milipuko ya kujirudiarudia ilibadili mfumo wa Ikolojia wa dunia.