Vijidudu vya malaria vilivyo 'sugu dhidi ya dawa ya artemisinin'

Mbu

Chanzo cha picha, Getty Images

Wanasayansi nchini Rwanda wamebaini kuwepo kwa usugu wa vijidudu ya malaria dhidi ya dawa ya kupambana na ugonjwa huo.

Utafiti , uliochapishwa kwenye jarida la Nature, umebaini kuwa vijidudu vilionesha usugu dhidi ya dawa ya artemisinin- dawa iliyo mstari wa mbele ya kupambana na ugonjwa wa Malaria.

Hii ni mara ya kwanza kwa wanasayansi kubaini usugu huo kwa dawa ya artemisinin barani Afrika.

Watafiti wanatahadharisha kuwa hali hii ''itasababisha tishio kubwa kiafya'' barani Afrika.

Wanasayansi kutoka taasisi ya Pasteur, wakishirikiana na Mpango wa taifa wa kudhibit Malaria nchini Rwanda, Shirika la Afya duniani (WHO), Hospitali ya Cochin na Chuo Kikuu cha Columbia (New York Marekani) wametathimini sampuli za damu kutoka kwa wagonjwa nchini Rwanda.

Waligundua mabadiliko katika vijidudu, usugu dhidi ya dawa ya artemisinin, katika wagonjwa 19 kati ya 257 au asilimia 7.4 ya wagonjwa katika moja kati ya vituo vya afya vilivyokuwa vikifuatiliwa.

Mabadiliko ya vijidudu

Katika jarida wanasayansi wametahadharisha kuwa vijidudu vya malaria ambavyo vilikuwa sugu dhidi ya dawa za awali '' zilikisiwa kusabisha ongezeko la mamilioni ya vifo vya watoto barani Afrika katika miaka ya 1980.''

Wakati dawa ya kwanza ya malaria, chloroquine ilipotengenezwa, wanasayansi walifikiri kuwa ugonjwa huo utatokomezwa ndani ya miaka kadhaa.

Lakini tangu miaka ya 1950 vijidudu hivyo vimekuwa vikijitengenezea usugu dhidi ya dawa hizo zilizoonesha mafanikio katika kupambana na vijidudu vya malaria.

Mchambuzi na mwanahabari wa masuala ya afya James Gallagher anasema kuwa hali hii inaogopesha.

Usugu dhidi ya dawa ya artemisinin sio kitu kipya kwa kuwa imekwishajitokeza pia sehemu kadhaa za Kusini Mashariki mwa bara la Asia kwa zaidi ya muongo mmoja.

Katika baadhi ya miji, asilimia 80 ya wagonjwa wanaugua malaria, huku vijidudu vikiwa sugu dhidi ya tiba ya malaria.

Lakini kwa Afrika ni zaidi, watu 9 kati ya 10 wanakabiliwa pia na hali hiyo.

Matokeo ni kuwa, hatahivyo, malaria ni ugonjwa ambao unakuwa mgumu kutibika.

Presentational grey line

Malaria kwa sasa hutibiwa kwa muunganiko wa dawa mbili- artemisinin na piperaquine.

Lakini hapo kabla vijidudu vilianza kutengeneza usugu dhidi ya artemisinin pia- hii kwa mara ya kwanza ilirekodiwa mwaka 2008 Kusini Mashariki mwa Asia.

Wakati huo wanasayansi walihofia kuwa usugu dhidi ya dawa hiyo utatokea pia kwa Afrika na kuwa hali hii inaweza kusababisha athari kubwa sana.

Mwaka 2018, nchi za Afrika zilirekodi vifo karibu asilimia 90 ya zaidi ya vifo 400,000 kutokana na malaria.