Hong Kong: Waandamanaji waanza kukamatwa chini ya sheria mpya ya kupinga maandamano

Muda wa kusoma: Dakika 5

Polisi huko Hong Kong wameanza kukamata watu kwa mara ya kwanza chini ya sheria mpya inayopinga maandamano.

Sheria hiyo ambayo imepitishwa na China, wakati imeanza kutekelezwa siku ambayo raia wa Hong Kong wanaandimisha miaka 23 tangu kumalizika kwa utawala wa Uingereza.

Watu saba wamekamatwa wakishtumiwa kukiuka sheria hiyo ikiwemo mwanaume mmoja aliyekuwa amebeba bendera ya wanaopendelea uhuru.

Takriban watu wengine 200 wamekamatwa katika mkutano uliokuwa umepigwa marufuku.

Sheria ya usalama wa taifa inalenga wanaotaka kujitenga, waasi na magaidi wakikabiliwa na adhabu ya hadi kifungo cha maisha.

Hata hivyo wanaharakati wanasema kwamba inakandamiza uhuru lakini China imekanusha ukosoaji huo.

Utawala wa Hong Kong ulikabidhiwa China na Uingereza 1997 na kuna baadhi ya haki ambazo zilitarajiwa kuanzishwa kwa angalau miaka 50 chini ya makubaliano ya nchi moja, mifumo miwili".

Kwa sasa hivi Uingereza imesema itatoa uraia kwa raia wa Hong Kong wenye pasipoti ya Uingereza.

Jumatano, maelfu ya raia wa Hong Kong walikusanyika katika mkutano wa kila mwaka unaopendelea demokrasia kuadhimisha kumalizika kwa utawala wa Uingereza ambao na kukiuka marufuku ya serikali ya mikusanyiko ya watu zaidi ya 50 kama njia moja ya kukabiliana na janga la corona.

Polisi wametumia mabomu ya machozi na majimaji yenye pilipili dhidi ya waandamanaji.

Walisema kwamba zaidi ya watu 300 wamekamatwa, tisa chini ya sheria mpya, ambayo ilianza kutekelezwa baada ya kutokea kwa maandamano makubwa yaliyosambaa kote Hong Kong mwaka jana.

Polisi imesema kuwa afisa mmoja amedungwa kisu mkononi na waandamanji waliokuwa na kifaa chenye ncha kali.

Sheria hiyo inasemaje?

Watu wa Hong Kong wanaweza kukutana na kifungo cha maisha jela kama watavunja sheria mpya ya usalama ambayo imewekwa na China.

Sheria hiyo imeanza kutekelezwa siku ya Jumanne lakini maelezo kamili ya sheria hiyo yalitolea saa kadhaa baadae.

Sheria hiyo ililetwa na China kufuatia ongezeko la ghasia na kuongezeka kwa harakati za demokrasia.

Wakosoaji wanasema sheria mpya ikifuatwa ipasavyo itapunguza maandamano na kuminya uhuru wa Hong Kong.

Eneo hilo ambalo lilirudishwa kwa China kutoka kwa utawala wa Uingereza mwaka 1997, lakini chini ya makubaliano ya kulinda uhuru wa raia wa eneo hilo ambao hawaufurahii - ukiwemo uhuru wa kujieleza.

Kiongozi wa Hong Kong, Carrie Lam, ametetea sheria hiyo akisema inasaidia kuondoa utofauti uliopo katika usalama wa taifa.

Maelezo yamekuwa yakilindwa kwa karibu na huku wanasiasa wa China wanakiri kuwa hawezi kusema chochote kwa kuwa hajaona rasimu ya sheria hiyo.

Lakini Ted Hui, mbunge kutoka upinzani ameiambia BBC: "Haki yetu imechukuliwa; uhuru wetu umeondoka; Sheria yetu , uhuru wa mahakama pia umeondoka."

Uingereza, Umoja wa Ulaya na washirika wa Nato wameelezea masikitiko yao wakati makundi ya kupambania demokrasia yalipoanza kuondoa hofu ya kulipiza kisasi kwa haraka.

Marekani pia imeitaka China kuzingatia kuwa tayari ilishaanza kuacha kuiangalia Hong Kong kiupekee ikiwemo kufurahia biashara na kusafiri nchini Marekani, ili kuirejeshea mamlaka China.

Tunafanyaje katika sheria?

Maelezo ya kina kuhusu sheria mpya yametolewa muda mfupi baada ya uzinduzi wa sheria hiyo.

Sheria hiyo inalenga wakazi wa kudumu na wasio wakudumu.

Haya ni baadhi ya maelezo yake:

  • Uhalifu wa kisiasa, kudharau mamlaka, ugaidi na kuungana na vikosi vya kigeni ni makosa ambayo yatahukumiwa kwa adhabu ya kuanzia miaka mitatu mpaka kifungo cha maisha.
  • Kuhamasisha chuki dhidi ya serikali ya China na serikali ya Hong Kong, ni makosa ambayo yanahukumiwa chini ya kifungo cha sheria namba 29
  • Uharibifu wa usafiri wa umma utatambuliwa kama ugaidi - waandamanaji mara nyingi huwa wanalenga kuharibu miundo mbinu ya mji wakati wa maandamano.
  • Wale ambao watakutwa na hatia hawataruhusiwa kukaa katika kituo cha polisi
  • Beijing itaanzisha ofisi mpya ya usalama mjini Hong Kong, ikiwa na sheria zake binafsi ambazo zitakuja katika mamlaka ya serikali
  • Mkuu wa Hong Kong amemteua jaji wa kesi ya usalama wa kitaifa na katibu wa sheria kuamua kama kuna hukumu au la.
  • Maamuzi ambayo yaliwekwa na tume ya usalama ya taifa , iliyowekwa na mamlaka ya wenyeji haiwezi kupingwa kisheria.
  • China wanasema pia wamechukua baadhi ya kesi ambazo zimeonekana kuwa muhimu sana , wakati mashtaka mengine yatasikilizwa wakati mlango ukiwa umefungwa.
  • Utawala wa kigeni wa taasisi zisizo za kiserikali na wakala wapya watawezeshwa
  • Sheria inaweza kuonekana kuwa inavunjwa kutoka kwa watu wa nje ambao sio wakazi wa eneo hilo, chini ya kifungu cha sheria namba 38
  • Sheria haitaweza kutekelezwa kabla haijapitishwa.

Chini ya sheria ya kitaifa , matukio mengi ya waandamanji ambayo yalitokea Hong Kong na kushangaza watu kwa zaidi ya mwaka yatachukuliwa kuwa ni uvunjwaji wa sheria na adhabu yake itakuwa kifungo cha maisha.

Kiongozi wa mji huo wa China, bwana Carrie Lam,alisema kuwa sheria ilikuwa imepita muda wake.

Kuhofia athari zake, wanaharakati wa kisiasa wanaachia wadhifa zao na kuwa watetezi wa waandamanaji,ambao wamewataka wasijitambulishe bado, na watu wa kawaida wameanza kufuta ujumbe wao kwenye mitandao ya kijamii.

Watu wengi wameacha kuzungumzia masuala ya kisiasa na kuacha kuzungumzia uhuru na demokrasia kwa sababu wanataka kuokoa maisha yao .

Wanataka kuokoa uhuru wao na kuzuia wasije wakafungwa.

Wakili mmoja ambaye ni mwanaharakati wa haki za binadamu pia alituma ujumbe mfupi muda ,mfupi tu baada ya sheria hiyo kupita lakini alitaka mawasiliano yote aliyoyaandika yafutwe kwa haraka.

Picha za mitandao ya kijamii inaonesha bendera inayotumiwa na maafisa kuonya waandamanaji kuhusu sheria mpya. Maafisa 4,000 walikuwa tayari kukabiliana na maandamano, gazeti la South China Morning Post limesema.

Sheria hiyo imepokelewaje?

Mara tu Sheria ilipopitishwa , wiki sita zilizopita ambapo ilitangazwa na kusainiwa na rais wa China bwana Xi Jinping.

Wanaharakati wa demokrasia walianza kuacha harakati kwa haraka wakiwa na hofu ya sheria mpya na hukumu ambayo itakayotolewa.

Wafanyabiashara ambao walikuwa wanawaunga mkono walianza kuondoa ushaidi wowote ambao ungewahusisa kuunga mkono waandamanaji.

Joshua Wong, katibu mkuu na muasisi wa kundi la pro-democracy Demosisto, ametoa angalizo kuwa mji utabadilika kuwa jimbo la siri la polisi.

"Beijing imeihaidi dunia kuwa Hong Kong itakuwa na kiwango cha juu cha uhuru ambao utathibitishwa kuwa ni uongo," kiongozi wa upinzani Ted Hui aliiambia BBC.

Lakini pamoja na hatari zake , baadhi watasalia kufungwa kwa kwa kuwa wanalenga kuendeleza mpango wao wa kufanya maandamano Julai, mosi, ripoti zinaeleza kuwa kikosi kikubwa cha polisi kimekusanyika katika mji wa Hong Kong.

Hatua ambayo imechochea mataifa ya kigeni kuhoji, katibu wa wizara ya mambo ya nje wa Uingereza bwana Dominic Raab, alisema China imevunja makubaliano ambayo walihaidiana juu ya watu wa Hong Kong katika makubaliano ya mwaka 1997 walipowarudishia eneo hilo.

Aliongeza kuwa serikali ilikuwa ina mpango wa kubadili sheria ya visa, ili kuruhusu mamilioni ya raia wa Hong Kong kupata uraia wa Uingereza.

Makubaliano yanalindwa na nchi , mifumo miwili iko kwenye nakala ambazo zinaitwa kuwa sheria za msingi ambazo ziko kwenye katiba ya - Hong Kong - kwa miaka 50.

Sheria za msingi kama ya uhuru wa kujieleza kama zipo au hazipo katika mji huo na mfumo wa serikali katika eneo hilo.

Julian Braithwaite, balozi wa Uingereza katika Umoja wa mataifa huko Geneva,aliliambia baraza la haki za binadamu la Umoja wa mataifa kuangalia kama sheria iko wazi katika suala la haki za binadamu.

Bwana Braithwaite, alizungumza kwa niaba ya mataifa 27, na kuitaka China kuzingatia hilo.