Mary Trump: Kumbukumbu ya mpwa wa rais Donald Trump inayomdhalilisha rais huyo

The Trump family siblings

Chanzo cha picha, Trump Campaign

Maelezo ya picha, Picha ya ndugu zake Trump, kutoka kushoto: Robert, Elizabeth, Fred, Donald na Maryanne

Mpwa wake rais wa Marekani Donald Trump amepanga kuchapisha kitabu kinachoelezea yote kumuhusu. Lakini je kwanini akaamua kufanya hivyo na mbona akaamua kujitokeza sasa?

Tarehe 28 Julai, Mary Trump amepanga kutoa kitabu alichokiita 'Too Much And Never Enough: How My Family Created the World's Most Dangerous Man', kampuni ya Simon & Schuster ilitangaza Jumatatu.

Kitabu hicho kitakua katika maduka ya vitabu wiki kadhaa kabla ya Mkutano Mkuu wa kitaifa wa chama cha Republican-Republican National Convention, wakati mjomba wake atakapokua akikubali ombi la uteuzi kwa ajili ya nia yake ya kutaka kuchaguliwa kwake tena kuiongoza Marekani mwezi Novemba.

Kitabu hicho kinaripotiwa kuwa kitafichua jinsi mpwa wake alivyolipatia gazeti la New York Times nyaraka za ushahidi wa siri ili litoe nakala za uchunguzi wa fedha binafsi za Bwana Trump.

Uchunguzi uliofanywa na taasisi ya Pulitzer Prize- unadai rais alihusika katika miradi ya "udanganyifu" wa kodi na kupokea zaidi ya dola milioni 400 (£316m) kutokana na biashara ya yake ya nyumba za makazi za baba yake.

Maelezo mafupi kuhusu kitabu yaliyotolewa na kampuni ya Amazon yanasema muandishi ataonyesha jinsi mjomba wake "alivyokua mwanaume ambaye sasa anatishia afya ya dunia, usalama Uchumi na jamii ".

"Anaelezea jinsi matukio kadhaa na familia kwa ujumla vilivyomtengeneza mwanaume aliyeharibika ambaye kwa sasa anaishi katika ofisi ya Oval Office, ikiwa ni pamoja na uhusiano wa kushangaza na wenye madhara kati ya Fred Trump na watoto wake wenyewe wawili wakubwa, Fred Jr na Donald," imeendelea kuelezea taarifa hiyo.

Taarifa hiyo fupi kuhusu kitabu cha mpwa wa Trump inasema mwandishi atatoa maelezo juu ya yale anayoyafahamu kama " shahidi wa kwanza aliyeshiriki milo isiyoweza kuhesabika nyakati za mapumziko na mwandani wa familia".

Kitabu hicho pia kitamshutumu rais kwa kuwa " kumkimbia na kumdharau " baba yake wakati alipoanza kuugua maradhi ya ubongo-Alzheimer's.

A photo of the Trump siblings during their younger years

Chanzo cha picha, Instagram/Donald Trump

Maelezo ya picha, Donald Trump akiwa mvulana kushoto kabisa) akiwa na ndugu zake Fred, Elizabeth, Maryanne na Robert

Mary Trump, mwenye 55, ni mtoto wa Fred Trump Jr, kaka mkubwa wa rais Trump, aliyefariki dunia 1981 akiwa na umri wa miaka 42.

Alihangaika na uraibu wa kupindukia wa pombe, kwa muda mwingi wa maisha yake na kifo chake cha mapema kilisababishwa na shinikizo la damu lililohusishwa na unywaji wake wa pombe.

Rais Trump alielezea kuwa matatizo ya kaka yake binafsi yanasukuma utawala wake kukabiliana na tatizo la uraibu wa pombe

Katika mahojiano aliyoyafanya mwaka jana na gazeti la Washington Post, Bwana Trump alisema alijuta kumshinikiza kaka yake mkubwa kujiunga na biashara ya nyumba wakati alipokua anafuata ndoto zake za kuwa rubani wa ndege.

Mary Trump amekua akiepuka kwa kiasi kikubwa kuonekana hadharani tangu mjomba wake awe rais, ingawa aliwahi kuwa mkosoaji wake hapo nyuma.

Uhasama mbaya baina yao ulianzia takriban miaka 20 iliyopita wakati yeye na kaka yake walipowasilisha kesi mahakamani dhidi ya mjomba wao na ndugu zake.

Maelezo ya video, President Trump spoke in 2017 about his brother's battle with alcoholism

Mnamo mwaka 2000, Mary Trump na Fred Trump III walipeleka mashtaka mahakamani juu ya mzozo wa pesa walizoachiwa za biashara ya nyumba ya baba yake Donald Trump , Fred Trump Sr.

walisema kuwa wosia wa mwaka 1991 "ulitengenezwa kwa udanganyifu na kwa ushawishi " kwa upande wa Donald Trump na ndugu zake, kwani wazazi wao upande wa baba waliugua maradhi ya ubongo kulingana na New York, Daily news.

Mary Trumpaliliambia gazeti la Jiji kwamba mashangazi na wajomba zake "wanapaswa kuaibika wenyewe " juu ya vita vya kisheria.

"Ikizingatiwa kuwa familia hii, huwezi kusema kuwa haijui lolote kuhusiana na pesa," aliliambia gazeti wakati huo.

Mary Trump na kaka yake waliwasilisha kesi baada ya bima yao ya matibabu inayotolewa na kampuni ya Trump kusitisha huduma kwao kama hatua ya kulipiza kisasi kwa hatua yao ya kwanza ya kisheria walioyoichukua dhidi ya Trump.

Hatimae kesi hiyo iulitatuliwa na maelezo ya kesi hiyo hayakutangazwa, kulingana na taarifa.

Donald and Fred Trump in 1988 at The Plaza Hotel in New York City

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Donald na baba yake, Fred, mnamo mwaka 1988 katika The Plaza Hotel- New York City

Rekodi za umma za jarida la People - People Magazine alizaliwa kwa Mary Lea Trump mwezi Mei mwaka 1965 na kuishi katika kisiwa cha Long Island, New York.

Ripoti za jarida la watu maarufu la Forbes alipata Shahada ya lugha ya fasihi ya kiingereza kutoka cha Tufts kilichopo Massachusetts na shahada ya juu katika somo hilo hilo kutoka Chuo Kikuu cha Columbia cha New York.

Pia alifanya Shahada ya Uzamivu -PhD katika saikolojia ya kliniki katika Chuo kikuu cha Adelphi University kilichopo New York.

Kulingana na maelezo ya utambulisho wa taaluma yake ambayo kwasasa yamefutwa kutoka katika wasifu mtandao wa LinkedIn, Mary Trump ni mshauri wa masuala ya kimaisha mwenye taaluma rasmi.

Mwaka 2012, aliripotiwa kuanzisha kampuni mjini New York iliyojulikana kama Trump Coaching Group. 

Wavuti wake unasema : "Je una matatizo ya kisaikolojia au unahisi hauna raha? Ukitafuta ukweli halisi wa maisha yako? Kama jibu ni ndio mshauri wetu wa masuala ya kimaisha anaweza kukuondoa katika hali hizo."

Kulingana na ujumbe wa Twitter uliokuwa na jina lake, Mary Trump anaonekana kuwa alikua mtu anayehisi kuwa asiye na furaha katika siku ya kuchaguliwa kwa mjomba wake Donald Trump mwaka 2016 .

Akaunti ya Twitter yenye jina lake ina ujumbe unaosema : "Huu ni mojawapo ya usiku mbaya zaidi katika maisha yangu."

Ujumbe mwingine wa Twitter ulimtaja hasimu wake wa Trump ambaye alimshinda katika uchaguzi huo , Hillary Clinton, "binadamu asiye wa kawaida na anayehedumia umma ". 

Katika ukurasa huo wa Twitter kuna kampeni ya kupinga ubaguzi wa rangi inayoendelea - Black Lives Matter, bendera ya wapenzi wa jinsia moja na nomino she/her/hers.