Virusi vya corona: Ni Kwanini baadhi ya makanisa bado yanafunguliwa msimu huu wa Pasaka?

Rais Trump alisema kuwa angependa kuona makanisa yakijaa watu Jumapili ya Pasaka. Hilo haliwezekani lakini sio yote yaliyofungwa.

Lakini je Pasaka inamaanisha nini huku janga la corona likiendelea?

Hilo ndio swali linalofanya wachungaji na makasisi wengi kujikuna vichwa nchini Marekani. Na pia limezua vita vya kisiasa juu ya haki ya kukusanyika majumbani kufanya ibada wakati ambapo nchini hiyo imetoa amri ya kutokusanyika katika maeneo ya umma kama njia moja ya kukabiliana na janga hilo.

"Tulikuwa tunafanya ibada ya kwenye mtandao kwa siku 15 za kwanza rais alizosema kwamba kutakuwa na marufuku hiyo," anasema James Buntrock, kasisi mshiriki wa kanisa la Glorious Way lililoko Houston, Texas.

"Lakini sasa baada ya kuingia wiki takatifu, Ijumaa ya matawi na sasa hivi ambapo Jumapili ya Pasaka inawadia, hiki ni kipindi maalum cha mwaka.

Pasaka ni moja ya tukio muhimu katika kalenda ya Kikristo. Linaleta pamoja mada zote zilizomo kwenye dini - matatizo, kifo, ufufuko na ukombozi. Na pia ni wakati ambapo idadi kubwa ya waumini hujumuika pamoja kanisani kufurahikia sherehe hiyo.

Makanisa mengi ya Marekani yameanza kutekeleza mashrati yaliyotolewa kukabiliana na corona kwa kuanza kutoa hudumu za mahubiri kwenye mitandai ya kijamii au kurekodi mahubiri.

Wengine wameanza kukutana katika maeneo yakuegesha magari na kadhalika.

Lakini wale ambao bado wanaendesha shughuli zao wanasema hawawezi kulinda waumini wako ka kuwapima kiwango cha joto, kunawa mikono kwa utumia vitakasa mikono (sanitizers) na kutowaruhusu wasikaribiane kwa umbali wa mita fiti 6.

Na katika majimbo angalau nane, mashirika ya kidini wameruhusiwa kutoka kaa nyumbani kama kitu cha lazima, baada ya kushinda kesi mahakamani.

Wabunge wa Kansas walifutwa amri ya gavana ya kupunguza mikusnayiko ya kidini hado 10.

Changamoto kubwa ni kutoka kwa wale ambao wanachukuliwa kuwa marufuku ya kufanya huduma ya kidini ni ukiukaji wa uhuru wa kuabudu kulingana na katiba, ingawa bado jadala kuhusu suala hili kisheria unaendelea.

Kwasababu ya usalama, Mhubiri Buntrock anasema atahisi kujukumika ikiwa mfuasi wake yeyote atapata virusi vya corona kwa kuhudhuria ibada kanisani kwasa tu kanisa hilo alijachukua hatua stahili," lakini akasisitiza kwamba kanisa hilo limechukua tahadhari.

Idadi kubwa ya wakiristo hawafikirii hilo.

Wanasema kwamba kutokwenda kanisani ndio hatua stahiki wanayopaswa kuchukua.

Mchungaji Nathan Empsall ni mmoja wao. Ni kiongozi wa kundi moja la wakiristo mashinani linalojiita Faithful America. Liliwasilisha kesi mahakamani likitaka makanisa yawache kuendesha shughuli zake kwa kukutana na watu ana kwa ana.

"Kusitisha kuabudu kwa mtu kuwa hapo, sio tu kulinda wale wanaokwenda kanisani ana kwa ana," anasema.

"Ni kulinda maisha ya kila mmoja, mfanyakazi wa dukani, stesheni ya gesi na mhudumu wa afya atakae kutana naye. Ukweli ni kwamba ni kuonesha upendo kwa jirani yak na uponaji kw amgonjwa, mambo ambayo Yesu alituamrisha kufanya."

Maneno yaliyotolewa na makamu rais wa Marekani Mike Pence mwaka huu kuhusu Pasaka alisisitizia umuhimu wa kuzingatia janga la corona.

Mhubiri Buntrock anashikilia msingi wa kuabudu pamoja kwamba ni muhimu katika kukabiliana na janga la corona kwasababu ya athari zake kiimani na kimwi vilevile.

"Watu wanapokusanyika pamoja kwa lengomoja, kuomba pamoja, mazingira, uwepo wa Mungu katika eneo hilo ni tofauti na yenye ngvu zaidi ikilinganishwa na watu wanaoomba wakiwa peke yao," amesema.

Wahubiri waliokiuka marufuku ya mamlaka ya kutotoka nje

  • mamia ya waumini walijitokeza kufanya ibada katika manisa la mhubiri wa Louisiana, Tony Spell, ambaye ameshtakiwa kwa kukiuka marufuku ya serikali. Alisema kwamba kanisa lake ni eneo la uponyaji
  • Mhubiri Rodney Howard-Browne wa kanisa la Megachurch huko Florida, pia naye anapambana na mamlaka baada ya kukiuka amri ya kusalia ndani huko Tampa Bay. Mbele ya umati wake alisema: "Ikiwa huwez kuwa salama kanisani, basi uopo kwenye matatizo makubwa mno"

Brooklyn, New York, eneo ambalo ni kitovu cha mlipuko wa corona, Mchungaji David Telfort ana mtizamo tofauti juu ya manufaa ya kiteolojia kipindi hiki.

Anajiuliza nini maana ya "kufurahia kuwa na matuamini katika ya kukata tamaa na kuomboleza".

"Hii ni fursa kwetu sisi kushikamana kipindi cha sikuku ya pasaka yenyehuzuni," amesema.

Lakini hata katika ufufuo, ingawam ni jambo la kipekee linakanganya.

Ukweli wa kwamba Wiki Takatifu inawadia huku dunia ikikabiliana na janga la Corona kutakuwa na hisia za huzuni.

"Tutamkumbuka vile alivyohisi Yesu katika bustani akiwa peke yake baada ya kutelekezwa na rafiki zake kwalioshikwa na usingizi, kama tulivyohisi kutenganishwa na rafiki zetu msimu huu," amesema Rev Empsall.

"Na Ijumaa Kuu, alikufa kwa uchungu mwingi msalabani. Rafiki zake kidogo tu ndo waliokuwa nae, vilevile, watu wanavyokufa peke yao hospitalini kwasasa."

Raia wa Marekani wikendi hii, wanasherehekea siku kuu ya pasaka kwa namna ambayo haijawahi kushuhudiwa hapo kabla. Na wengi pia watasikiliza simulizi na kushuhudia msimu huu wa pasaka kwa hisia za kuhuzunisha.