Coronavirus: Kuna uwezekano mkubwa wa watu nusu bilioni kuwa maskini

Farm labourers separate peanuts from their stems after they are harvested in Central Sulawesi Province, Indonesia.

Chanzo cha picha, Getty Images

Mdororo wa uchumi kwasababu ya virusi vya corona huenda ukaongeza kiwango cha umaskini duniani hadi nusu bilioni, kwa mujibu wa shirika la Oxfam.

Kwa kutumia utafiti uliofanywa na Chuo Kikuu cha Taifa cha Australia (ANU) na Kings College, London, shirika la Oxfarm limesema itakuwa mara ya kwanza kiwango cha umaskini kuongezeka kote duniani katika kipindi cha miaka 30.

"Mdororo wa kiuchumi kuna uwezekano mkubwa ndo ukaongezeka zaidi hata kuliko janga la afya linalokabili dunia," ripoti hiyo imesema.

Lilikadiria kwamba kuongezeka kwa idadi ya umaskini kati ya milioni 400 hadi 600 kote duniani.

Utafiti huo unawadia kabla ya mkutano mkuu wa benki ya Dunia, Shirika la Fedha Duniani na mkutano wa Mawaziri wa fedha kutoka nchi za G20 wiki ijayo.

Ripoti hiyo inasema athari za ugonjwa wa virusi vya corona ni changamoto kubwa kwa malengo endelevu ya Umoja wa Mataifa yaliyolenga kumaliza umaskini kufikia 2030.

Habari zaidi za Corona
Banner

"Utafiti wetu umezingatia umuhimu wa kuendelea kwa masuala ya kijamii katika nchi zinazoendelea haraka iwezekanavyo na angalizo kwa athari ya ugonjwa wa virusi vya Corona kwa nchi hizo na kile ambacho jumuiya ya kimataifa inaweza kufanya kusaidia," amesema Profesa Andy Sumner kutoka King's College London.

Janga hili likimalizika, nusu ya idadi ya watu kote duniani ambao ni bilioni 7.8 watakuwa wanaishi kwa umaskini. Takriban asilimia 40 ya watu wapya katika umaskini kuna uwezekano mkubwa wakawa ni kutoka Mashariki mwa Asia na Pasifiki, kukiwa na karibia theluthi moja ya watu kutoka eneo la Afrika na Kusini mwa Asia.

Mtendaji mkuu Danny Sriskandarajah, kutoka Oxfam amesema: "Kwa mabilioni ya wafanyakazi kutoka nchi maskini ambazo tayari zinapitia wakati mgumu, mambo ya msingi yanayohakikisha usalama wa kijamii kama vile mtu akilipwa akiwa mgonjwa na usaidizi kutoka kwa serikali tayari havipatikani.

"Mikutano ya wiki ijayo ya Benki ya Dunia na G20 ni fursa muhimu kwa viongozi wa dunia kushirikiana katika kunusuru uchumi kusaidia wale walio katika hatari zaidi."

Mapema wiki hii, zaidi ya mashirika 100 yalitoa wito wa kutaka nchi zinazoendelea ziruhusiwe kutolipa madeni yao mwaka huu ambako kunaweza kusaidia kupatika kwa hadi dola bilioni 25(£20bn) pesa taslim kusaidia uchumi wao.