Encephalitis: Ugonjwa uliosababisha amsahau mpenzi wake

Georgia Lee bado hawezi kukumbuka kuwa alisoma mamafunzo ya chuo kikuu .

Kwa muda, msichana huytu mwenye umri wa miaka 23- hakuweza kukumbuka chochote kumuhusu mpenzi wake wa kiume.

Georgia alipoteza miaka mitano ya kumbukumbu yake wakati alipopata ugonjwa encephalitis alipokua na umri wa miaka 22.

Ni ugonjwa unaotishia maisha unaosababisha kuvimba kwa ubongo kunakosababishwa na virusi vya aina fulani vinavyosambaa kote mwilini.

''Nilikua na maumivu ya kichwa muda wote kwa kipindi cha wiki mbili kwenye eneo moja tu la paji la uso," Gemma aliiambia Radio 1 Newsbeat nchini Uingereza.

"Hakuna tembe zilizoweza kunitibu. Halafu siku moja nilimtumia ujumbe wa simu mpenzi wangu ambao ulikua hauna maana yoyote ."

Wakati baba yake Georgia alipokuja kumtembelea, alibaini kuwa kuna kitu ambacho hakikuwa sawa na akamkimbiza hospitalini.

Kwanza , madaktari walifikiri alikua na ugonjwa wa uti wa mgongo lakini baada ya kupoteza fahamu ilibainika kuwa alikua na ugonjwa wa kuvimba ubongo encephalitis.

Inakadiriwa kuwa kila mwaka watu wapatao 500,000 hupata maradhi haya kote duniani na takriban 6000 kati yao.

Alipokua hospitalini na kuulizwa alikua ana umri wa miaka mingapi , Georgia alisema ana umri wa miaka wa miaka 17-kwasabu hakuweza kukumbuka chochote kuhusu maisha yake ya nyumba.

Georgia anasema bado anahisi ana chini ya miaka 23 na kumbukumbu yake bado haijarejea kikamilifu -na masomo yake ya chuo kikuu hakumbiki chochote alichokisoma.

Katika mchakato wake wa kupona sasa najifunza mambo madogo madogo ya kimaisha ambayo watu wengine wanayaona yakawaida , kama vile kupanda vyombo vya usafiri wa umma au kuwatembelea marafiki.

"Vitu vya kawaida kama vile kupanda basi mwenyewe, kwenda madukani au kwenda kwenye nyumba ya mtu ni hatua kubwa sana kwangu," anasema.

Pia ilimbidi afanye mtihani tena wa kupata leseni ya kuendesha gari kwasababu hakua na kumbukumbu ya kuendesha tena wakati alipokua na umri wa miaka 18.

Na pia imeathiri mahusiano yake pia na watu wengine.

Kwanza alianza kwa kushindwa kuelewana na mpenzi wake.

"Ilibidi kwanza nimfahamu tena kama ndio kwanza tumekutana kwa mara ya kwanza, sawa na marafiki zangu wote niliosoma nao chuo kikuu ," anasema Georgia.

" Kwa mara ya kwanza alikua ni mtu mwenye aibu hakujua afanye nini. Halafu akachukua muda kidogo. Alianza kuniambia kuhusu maisha yetu ya nyuma, kisha akanionesha

'Chakula ninachokula sasa ni kile nilichokua nikikichukia'

Ugonjwa wa Georgia wa acephalitis ulisababishwa na malengelenge lakini baada ya kusababisha kuvimba kwa midomo yake, ulikwenda hadi kwenye koo kabla ya kwenda kwenye ubongo.

Athari zake ni tofauti lakini sambamba na kupoteza kumbukumbu, Georgia alipoteza uwezo wa kutambua harufu na ladha hadi sasa.

"Sina uwezo wa kutambua harufu kabisa. Ninaweza kutambua ladha ya chakula chenye viungo vingi sana lakini ni hilo tu. Hivi karibuni niliagiza pizza yenye ladha ya nanasi katika mgahawa.

"Kimsingi chochote ninachoweza kutambua ladha yake ni chakula ambacho awali nilikichukia ."

Wakati anaposhindwa kuonja, Georgia huweka chochote katika supu yake iwe yenye pilipili au kechapu ili kuongeza ladha zaidi.

'Marafiki zangu wote tayari wamekwishapata kazi zao walizozipenda'

Encephalitis imechukua maisha yaliyopita ya Georgia, lakini sasa anahofu juu ya athari ambazo ugonjwa huu unaweza kumsababishia siku zijazo.

"Ninajaribu kuwa na mtizamo chanya lakini huwa ninajipata inakua rahisi kuwa na mtizamo hasi ," anasema , akiongeza kuwa kusaka kazi huku akiwa hakumbuki masomo yake ya Chuo kikuu ni changamoto kubwa.

''Kama sina chochote cha kusema kwao juu ya shahada yangu, sasa ni nini nichoweza kufanya kazini ?"

Pia imekua ni vigumu sana kuwasiliana na marafiki zake, ambao sasa wako katika maeneo tofauti katika maisha yao ikilinganishwa na maisha yake ya sasa.

''Wengi miongoni mwa marafiki zangu wamepata kazi zao, tayari wamepata nyumba zao na wapenzi wao, yote hayo'', anasema.

"Ninahisi tu kama itachukua muda mrefu hadi niweze kufanya hayo na kuendelea tena na kuweza kujiamini mwenyewe ."

Lakini Georgia ana matumaini juu ya maisha yake ya baadae na ana mtazamo chanya huku akiendelea kupona.

"Natamani ningekumbuka chuo changu kikuu. Lakini huwa ninahisi kila mara nina bahati kwamba ilikua ni miaka mitano tu na si kwamba maisha yangu yote yameenda."