Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Conovirus: Nigeria yathibitisha kuingia kwa corona, Afrika Kusini kuwaondoa raia wake Wuhan
Nigeria imethibitisha kuwepo kwa mtu mmoja mwenye maambukizi ya virusi vya corona.
Mgonjwa huyo, raia wa Italia anayefanya kazi nchini Nigeria alisafiri kwa ndege kwenda mji wa kibiashara wa Lagos akitokea Milan tarehe 25 mwezi Februari.
Mamlaka zinasema anaendelea vizuri na hakuna dalili ya hatari na hivi sasa anapatiwa matibabu hospitalini jijini Lagos.
Serikali ya Nigeria imesema ilijiandaa na kuwa imekuwa ikiandaa vituo kwa ajili ya operesheni za dharura, ili kuchukua hatua za udhibiti.
Mamlaka zimesema zimeanza kuwatambua wale wote waliokaribiana naye tangu aliporejea Nigeria.
Zaidi ya watu 80,000 wameripotiwa kuathirika katika nchi 40. Zaidi ya watu 60 wamepoteza maisha nje ya China, ambapo mlipuko ulipoanza. Hatahivyo, idadi ya maambukizi nchini China imeendelea kushuka
Afrika Kusini
Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa ameamuru kuondolewa kwa raia wa Afrika Kusini 132 wanaoishi mjini Wuhan.
Uamuzi ulitangazwa siku ya Alhamisi baada ya kikao cha baraza la mawaziri baada ya maombi ya wana familia wa raia hao wanaoishi Wuhan, ofisi ya rais imeeleza.
Haikuelezwa ni lini wataondoshwa huko lakini serikali imesema raia 132 kati ya 199 wanaishi mjini Wuhan wameomba warejee nyumbani.
Hakuna kati yao aliyegundulika kuathirika na virusi au kuwa na dalili za ugonjwa, lakini watawekwa kwenye karantini kwa siku 21 watakapowasili nchini Afrika Kusini kama ''hatua ya tahadhari'' ofisi ya rais imetangaza.
''Serikali imekuwa ikifanya mazungumzo na familia za walioathirika na idara zinazohusika zimekuwa zikifanya mipango muhimu kuwapokea,'' iliongeza.
Jeshi na wataalamu wa afya watatoa msaada wakati watakapokuwa wanawekwa karantini.
Shirika la ndege la Afrika Kusini, zimesitisha safari za moja kwa moja kwenda China.
Kwingineko barani Afrika, Algeria na Misri pia zimethibisha kuwepo kwa maambukizi.
Unaweza pia kusoma