Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Virusi vya Corona: Ufilipino yaripoti kifo cha kwanza cha mgonjwa wa corona
Mwanaume mmoja nchini Ufilipino amethibitika kufa nje ya China kutokana na virusi vya Corona.
Mgonjwa wa virusi hivyo vya corona alikuwa na umri wa miaka 44, raia wa China kutoka mji wa Wuhan, jimbo la Hubei eneo ambalo virusi vya kwanza vya corona vilibainika.
Alionekana kuwa muathirika wa virusi hivyo alipowasili Ufilipino, shirika la afya duniani (WHO) limesema.
Zaidi ya watu 300 wamefariki kutokana na mlipuko wa ugonjwa huo na wengi wakiwa wametokea Hubei. Zaidi ya watu 14,000 wameathirika mpaka sasa.
Marekani, Australia na mataifa mengine wameweka zuio la kupokea wageni kutoka China na kukubali raia wao kuwekwa karantini.
Idadi ya watu wenye virusi vya corona duniani kote imezidi maambukizi ya ugonjwa wa Sars ulivyokuwa, ambapo watu wengi walifariki dunia katika maeneo mbalimbali ya dunia mwaka 2003.
Lakini takwimu za vifo vya sasa zinaonyesha kuwa virusi vipya vya corona viko chini na sio hatari kwa kiwango hicho.
Tunafahamu nini kuhusu kifo hiki nje ya China?
Mwanaume huyo alikuwa akisafiri Ufilipino akiwa anatokea Wuhan na alipitia Hong Kong, alikuwa akiongozana na mwanamke raia wa China mwenye umri wa miaka 38 ambaye pia alipimwa na kukutwa na virusi vya corona.
Maofisa wanasema kuwa alikuwa amelazwa hospitalini katika mji mkuu wa Manila, eneo ambalo alionekana kuwa na dalili za ugonjwa huo.
Mwanaume huyo anadaiwa kuwa alikuwa na matatizo mengine ya kiafya.
Rabindra Abeyasinghe, muwakilishi wa shirika la afya, WHO nchini Ufilipino amewataka watu wawe watulivu: "Hiki ni kisa cha kwanza cha kifo cha virusi vya corona kumuua mtu nje ya China. Hata hivyo tunataka watu waelewe kuwa mtu huyo alifika na ugonjwa huo kutoka China na hakuupata ugonjwa huo akiwa Ufilipino."
Kwa mujibu wa vyombo vya habari nchini huo, wizara ya afya imesema kuwa mgonjwa huyo alikuwa anaonyesha dalili za kupona lakini hali ilibadilika ndani ya saa 24 tu.
"Tunafanya kazi na mamlaka ya ubalozi wa China ili kuhakikisha kuwa mwili wa marehemu unaangaliwa kwa umakini kulingana na viwango vya kitaifa na kimataifa vya kukabiliana na ugonjwa huo," bwana Duque alisema na kuongeza kuwa mwili wa mwanaume huyo utachomwa.
Idara ya afya inajaribu kufuatilia abiria ambao walipanda ndege moja na mtu huyo aliyekufa ili wawekwe kwenye karantini, pamoja na watu wengine ambao walikutana na mwanaume huyo katika hoteli au waliwasiliana na mtu huyo kwa namna moja au nyingine.
Awali kulikuwa na katazo kwa watu kutoka Hubei eneo ambalo mlipuko ulitokea kuingia katika nchi hiyo.
Nini kipya nchini China?
Mamlaka imesema kuwa watu zaidi ya 45 wamefariki katika jimbo la Hubei mpaka siku ya jumamosi, na kufanya vifo vya virusi vya corona kuwa 304.
Visa vipya vya ugonjwa wa corona vimethibitika kuwa 2,590. Jumla ya idadi ya waathirika wa ugonjwa huo China imefikia kuwa 14,380, televisheni ya taifa imenukuu baraza la taifa la afya.
Chuo kikuuu cha Hong Kong kimedai kuwa visa vya waathirika vinaweza kuwa viko juu zaidi ya takwimu ambayo inaelezwa.
Zaidi ya watu 75,000 wameathirika katika mji wa Wuhan, eneo ambalo mlipuko wa ugonjwa wa corona uliibuka.
Hospitali mpya itaanza kulaza waathirika wa ugonjwa wa corona kuanzia siku ya jumatatu, chombo cha habari cha taifa kimeripoti.
Hospitali hiyo imejengwa kwa ajili ya kusaidia na tatizo hilo la corona.
Siku ya jumapili, serikali itawekeza zaidi ya dola bilioni 170 ili kukabiliana na janga hilo.
Mataifa gani wameweka zuio la virusi vya corona?
Marekani na Australia zimesema kuwa watakataa wageni wote ambao watafika nchini mwao wakiwa wametokea China hivi karibuni.
Mataifa mengine ni New Zealand, Urusi, Japan, Pakistan, Iraq, Italia, Indonesia na Singapore pia wameweka katazo la kuzuia watu kusafiri kwenda China na kuingia nchini mwao wakitokea China.
Siku ya jumapili, Korea kusini pia watakataza wageni wote watakoingia wakiwa wametokea Hubei.
Raia wa Marekani ambao watakuwa wamerejeshwa kutoka Hubei watawekwa kwenye karantini kwa muda wa siku 14.
Zuio la watu kusafiri linasaidia?
Maafisa wa afya wameshauri kuhusu zuio hilo.
"Katazo la watu kusafiri linasababisha watu kuingia kwenye matatizo zaidi, kwa sababu watu wanakosa taarifa, usambazaji wa madawa unakuwa duni, uchumi unashuka na hata watu wanatafuta njia ambaozo si rasmi kuondoka katika eneo lililoathirika, mkuu wa shirika la afya alisema siku ya ijumaa.
WHO alishauri kuwa watu wanapaswa kupimwa wakiwa mpakani wakati wanasafiri.
Kwa sababu hatua ya kufunga mipaka inafanya watu kutumia njia za panya kutoka eneo moja kwenda lingine.
China imekosolewa kwa zuio hilo la watu kusafiri.
Mataifa mengine yamechukua hatua gani?
- India imewarudisha raia wake 300 kutoka Wuhan. Wajerumani takribani 100 wamerejeshwa nyumbani kutoka China. Thailand na Urusi wamewaondoa raia wake kutoka Wuhan na jimbo la Hubei
- China ameitaka umoja wa ulayakusaidia kusambaza madawa katika mataifa mengine.
- Mashirika kadhaa ya ndege kama Qantas, Air New Zealand, Air Canada naBritish Airways, zimesitisha ndege kutokea China.
- Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un ametuma barua ya rambirambi kwa rais wa China.
- Hoteli mbalimbali zimeweka sera za kutopokea wageni kutoka China, zikiwemo Hyatt, Radisson naHilton.
- Apple imesema kuwa itasitisha kutoa taarifa za China kwa muda
- Urusiimesema kuwa raia wawili wa China wamepimwa na kukutwa na virusi na kuwatenga .
- Ujerumani, Italia naSweden imethibitisha kuwa na visa vya ugonjwa huo barani ulaya.