Uchunguzi dhidi ya Trump: Rais aandika barua ya hasira kwa Spika Pelosi

Chanzo cha picha, AFP
Rais Donald Trump ameukosoa uchunguzi unaokaribia kufanyika kwa barua ya hasira kwa afisa wa ngazi ya juu wa Democrat Spika Nancy Pelosi, akimtuhumu kwa kutangaza "vita vya wazi dhidi ya demokrasia ya Marekani".
"Umeshushia hadhi umuhimu wa neno Uchunguzi!" aliandika katika barua iliyotumwa Jumanne.
Bwana Trump anakabiliwa na kura ya uchunguzi Jumatano kuhusu madai kwamba aliishinikiza Ukraine kwa ajili ya maslahi binafsi ya kisiasa.
Anatarajiwa kufanyiwa uchunguzi, utakaoandaa kesi katika bunge la Senati.
Huku kukiwa na matumaini kidogo ya kubadili matokeo ya kura ya uchunguzi huo Jumatano katika bunge, Bwana Trump alitumia barua yake ya kurasa sita kuonyesha hasira yake dhidi ya mchakato na kumpinga Bi Pelosi , ambaye ni Spika wa bunge anaetoka katika chama cha Democrat.
Ilikua ni hatua isiyo ya kawaida iliyochukuliwa na rais , ambae alipigana kuzuia mchakato wa kumchunguza kwa kuwazuia washirika muhimu kutoa ushahidi katika Bunge la wawakilishi.
Bwana Trump anadai katika barua yake kwamba "alinyimwa haki ya kimsingi ya kikatiba kuanzia mwanzoni mwa mchakato wa uchunguzi" na "kunyimwa haki za kimsingi zinazotolewa na katiba , ikiwemo haki ya kuwasilisha ushahidi."
"Haki ya mchakato ilitolewa zaidi kwa wale walioshitaki katika kesi ya Salem Witch Trials," aliandika.
Ukweli ni kwamba rais alialikwa wazi na mwenyekiti wa Kamati ya Sheria ya Bunge kutoka chama cha Democrat kutoa ushahidi katika mchakato wa uchunguzi huo, jambo ambalo lingeruhusu timu yake ya kisheria kuwahoji mashahidi, lakini alikataa.
Meya wa Salem, Kim Driscoll, alituma ujumbe wa Twitter kwamba rais anapaswa "kujifunza historia," akisema kuwa kesi za kichawi zilizowapata na hatia wahusika zilifanyika wakati hakuna ushahidi, huku kesi dhidi ya rais ikiwa na "ushahidi wa kutosha."

Chanzo cha picha, Twitter
Bi Pelosi aliwaambia waandishi wa katika Bunge kwamba alikua bado hajaisoma barua ya rais kamili lakini ameona "dhana" yake na anafikiri "ina matatizo".
Katika taarifa iliyotangaza kura ya Jumatano juu ya uchunguzi, alisema Bunge lita "tekeleza moja ya mamlaka yake makubwa tunayopewa na katiba''.
"Katika kipindi hiki cha maombi katika taifa letu , lazima tuheshimu kiapo chetu cha kuunga mkono na kulindakatiba yetu dhidi ya maadui wote, wa kigeni na wa ndani ya nchi ," aliongeza.
Bwana Trump anakabiliwa na mashtaka mawili katika uchunguzi: Kuzuia utendaji wa bunge la kongresi , kwa kukataa kushirikiana na uchunguzi , kuwazuiawafanyakazi kutoa ushahidi, na kuficha ushahidi wa nyaraka ; na kujaribu kutumia ofisi yake kuishinikiza Ukraine kumchunguza hasimu wake wa kisiasa kutoka chama cha Democratic Joe Biden.

Chanzo cha picha, Drew Angerer/Getty Images
Ikiwa kura ya bunge kama inavyotarajiwa Jumatano sambamba na mirengo ya kisiasa, Bwana Trump atakua rais wa tatu katika historia ya Marekani kuchunguzwa. Baadae atashtakiwa katika Senati, ambako maseneta kutoka vyama vyote wanapaswa kutekeleza wajibu wao wa kutoa hukumu kwa uhuru.
Bunge la Seneti linadhibitiwa na chama cha rais cha Republican . Kiongozi wa sebeti Mrepublican Mitch McConnell aliwaudhi Democrats wiki iliyopita aliposema maseneta wa Republican watashughulikia uchunguzi wa Trump kwa "uratibu kamili" na timu ya rais wakati wa kesi na kupiga kura kupinga mchakato.
Chuck Schumer, Kiongozi wa walio wachache katika bunge la Seneti alisema : " Kama vipengele vya uchunguzi vitatumwa katika Senati, kila Seneta atakula kiapo cha kutoa 'haki bila upendeleo '.
Kuhakikisha Seneti inaendesha kesi ya haki na ya kweli inayoruhusu ukweli wote unajitokeza ni jambo muhimu ."
Mapema Jumanne, Wakili binafsi wa Bwana Trump Rudy Giuliani alionekana kuthibitisha kwamba alifanya juhudi za kumuondoa balozi wa marekani nchini Ukraine, Marie Yovanovitch, ili kutoa fursa kwa ajili ya uchunguzi hilo linaweza kuwa jambo la maana kisiasa kwa Bwana Trump.
Bwana Giuliani aliliambia gazeti la New York Time kuwa alimfikishia Bwana Trump "mara kadhaa" taarifa juu ya namna Bi Yovanovitch anaweza kuwa alihusika kwa njia fulani katika uchunguzi.
"Nilihitaji Yovanovitch atoke," Bwana Giuliani aliliambia gazeti hilo la New York.















