Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Mafuriko ya Afrika mashariki: Jinsi mvuvi huyu wa Kenya alivyookolewa na ndege katika mafuriko
Mvuvi mmoja amenusuriwa kutoka kwa kisiwa ambacho alikuwa amekwama tangu siku ya Ijumaa kutokana na mafuriko makali.
Vincent Musila alikuwa amekwenda kuvua samaki kama kawaida katika mto mmoja mjini Thika katikati mwa Kenya wakati mto huo ulivyovunja kingo zake.
Watu wengi walitazama bila usaidizi wowote walipokuwa wakisubiri usaidizi wa dharura ili kumuokoa.
Zaidi ya watu 250 wameuawa na wengine milioni kuathiriwa na mafuriko na maporomoko katika eneo lote la Afrika mashariki.
Takriban nusu ya vifo 120 vimetokea nchini Kenya huku zaidi ya watu 160,000 wakiathiriwa.
Bwana Musila anasema kwamba mafuriko hayo yalianza ghafla kutoka katika eneo moja lililiopo katikati ya mto huo , nje ya mji wa Thika.
''Sekunde chache baadaye kulikuwa na maji kila mahali nikashindwa kuvuka''.
''Hali imekuwa mbaya katika kipindi cha siku tatu katikati baridi na mvua. Nilikuwa na njaa na nilifikwa na mambo mengi''.
"Kulikuwa na mbu chungu nzima na nilikuwa nikiogopa wanyama kama vile mamba na kiboko . lakini nafurahi na najihisi vyema baada ya uokoaji huo.
Nahisi kana kwamba nimezaliwa upya, aliambia chombo cha habari cha NTV nchini Kenya''.
Makundi ya watu waliokongamana kandokando ya mto huo walifurahia wakati ndege aina ya helikopta ya maafisa wa polisi ilipowasili kumnusuru,
Mwandishi wa BBC Emmanuel Igunza anasema kwamba baadhi ya raia hao walimchukua manusura huyo na kumpeleka katika mkahawa ambapo alikula viazi karanga na sausage - ikiwa ni chakula chake cha kwanza katika kipinid cha siku tatu.