Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Maandamano dhidi ya mauaji ya maafisa wa Ebola huko Ituri yafanyika DRC
Shambulio hilo la mapema alfajiri Wanaharakati kutoka kundi moja la kupigania haki za kibinadamu LUCHA (Lutte Pour Le Changement, or 'struggle for change'), na wale wa Oparesheni Filimbi (Whistle Blowers) wamekongamana katika mji wa Goma katika afisi ya ujumbe wa Umoja wa mataifa UN nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo kupinga mauaji dhidi ya wafanyakazi watatu wa Ebola ambao ni wenyeji.
Shambulio hilo katika vituo viwili vya matibabu lililofanyika katika eneo la Ituri linadaiwa kutekelezwa na waasi wa Maimai ambao ni wapiganaji kutoka eneo hilo.
Wanaharakati hao pia wamekasirishwa na mauaji ya wanakijiji 19 katika kijiji cha Maleki, mjini Beni karibu na mpaka na Uganda.
Shambulio hilo linadaiwa kutekelezwa na waasi wa ADF.
Wanasema serikali na Umoja wa mataifa wamewaacha raia chini ya usimamizi wa washambuliaji hao.
Kiongozi wa kitengo cha dharura dhidi ya ugonjwa wa Ebola nchini DRC Jean Kacques Muyembe ametaja mashambulio ya vituo hivyo viwili na mauaji hayo ya wahudumu watatu kuwa pigo kuu.
Bwana Jean amesema kwamba atafanya mazungumzo na vyombo vya habari muda wowote kuanzia sasa ili kuelezea kuhusu hali ilivyo.
Mapema siku ya Alhamisi waasi hao walivishambulia vituo viwili vya matibabu vya Ebola vinavyoendeshwa na Shirika la Afya Duniani (WHO), katika uvamizi uliofanyika usiku wa kuamkia Alhamisi na kuwauwa wahudumu watatu.
Taarifa zinasema kuwa miongoni mwa watu waliouawa ni wafanyakazi wa WHO na kwamba watu wengine wanne wamejeruhiwa vibaya.
Kwa mujibu wa mashuhuda, waasi waliwazidi nguvu polisi kwenye vituo hivyo vilivyopo katika maeneo yaMangina na machimbo ya Biakato.
Magari manne yamechomwa moto pamoja na majengo kadhaa yameteketezwa.
Kupitia ujumbe wake wa Twitter, maafisa wakuu wa shirika hilo akiwemo Mkurugenzi Mkuu Bwana Tedros Adhanom Ghebreyesus wamelaani shambulio hilo lililosababisha vifo na majeruhi:
Hii si mara ya kwanza kwa mashambulio ya aina hii kutokea katika vituo vya Ebola nchini humo.
Mashambulio ya wanamgambo na ukosefu wa imani ya jamii kwa wafanyakazi wa afya mashariki mwa Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Kongo yamekuwa ni kikwazo cha juhudi za kudhibiti mlipuko wa hivi wa Ebola ambao ni hatari kwa taifa hilo na mataifa mengine jirani.
Makundi ya waasi yenye silaha yamekuwa yakishambulia mara kwa mara vituo vya tiba ya Ebola, huku kukiwa kuna ukosefu wa imani miongoni mwa jamii za wakazi wa maeneo yaliyoathiriwa na Ebola ambao wanalaumu wageni kwa mlipuko wa maradhi hayo.
Hali hiyo inachangia juhudi za kukabiliana na mlipuko huo kuwa ngumu katika majimbo yenye mizozo ya Ituri na Kivu.
Shirika la kuhudumia wakimbizi UNHCR lilisema kuwa watu 300,000 wamesambaratika kufuatia ghasia katika eneo hilo katikakipindi cha mwezi huu pekee.
Unaweza pia kusoma:
Kipindi cha mashambulio dhidi ya wahudumu wa afya na vituo
Umoja wa Mataifa umeripoti zaidi ya matukio 174 ya ghasia zinazoathiri wafanyakazi na vituo vinavyotoa huduma za dharura za Ebola katika majimbo ya Ituri na Kivu kaskazini tangu ulipoanza mlipuko.
Mashambulio ya mwaka 2018:
- Septemba 22-24: Uvamizi wa vikosi vya waasi wa Uganda wa Allied Defence Forces (ADF) mjini Beni, Kivu Kaskazini ambapo watu 18 walikufa na kusababisha maandamano ya kuvurugwa kwa shughuli za kukabiliana na Ebola.
- Oktoba 20: Watu kumi na wawili waliuawa katika shambulio la ADF katika mji wa Beni na kuvuruga shughuli za kukabiliana na Ebola kwa siku kadhaa.
- Oktoba 23 : Wauguzi wawili kutoka kitengo cha tiba cha Jeshi la DRC (FARDC) waliuawa katika mji wa Butembo tarehe 22 Oktoba
- Novemba 8: Wanamgambo wa Mayi-Mayi waliwateka kwa muda timu ya wahudumu wa kukabiliana na Ebola.
- Disemba 27:Wagonjwa walitoroka walitoroka wakati umati wa watu wenye hasira walipovamia kituo cha kupuma Ebola cha Beni.
- Februari 16: Wakazi walivamia kituo cha udhibiti wa Ebola katika jimbo la Ituri.
- Februari 24 : Watu wenye silaha waliteketeza kwa motokituo cha matibabu ya Ebola katika eno la Katwa, mjini Butembo.
- Februari 27: Afisa wa Usalama aliuawa na wagonjwa 31 walitoroka baada ya shambulio dhidi ya madaktari wasio na mpaka (MSF) katika kituo cha matibabu ya Ebola mjini Butembo.
- Machi 9 : Watu wawili, akiwemo afisa wa polisi waliuawa katika kituo cha matibabu ya Ebola katika mji wa Butembo.
- Machi 14: Mtu mmoja aliuawa katika shambulio la wizi katika kliniki ya Ebola katika ya Mamboa, eneo la Lubero , katika mkoa wa Kivu Kaskazini.
- Aprili 5: Watu wenye silaha walivamia na kupora ofisi za MSF yaliyopo katika eneo la Byakato, jimboni Ituri. Hakuna binadamu aliyeripotiwa kufa.
- Aprili 19 : Daktari wa Cameroon anayefanyia kazi shirika la afya Duniani WHO alipigwa risasi katika shambulio dhidi ya kliniki ya Chuo kikuu cha Graben (UCG) iliyopo mjini Butembo.
- Aprili 20: Shambulio lilifanyika katika Hospitali ya Katwa mjini Butembo na kuzimwa na vikosi vya usalama. Mshambuliaji akauawa.
- Mei 3: Shughuli za kukabiliana na Ebolaziliahirishwa mjini Butembo baada ya makabiliano baina ya waendesha pikipiki na timu iliyokuwa ikijaribu kusimamia mazishi salama ya wagonjwa wa Ebola.
- Mei 8: Maafisa wa kukabiliana na Ebola mjini Butembo walishambuliwa na wanamgambo wa Mayi Mayi ambapo washambuliajii kumi waliuawa. Shughuli hizo ndio kwanza zilikuwa zimefufuliwa baada ya kuahirishwa kwa siku tatu .
- Mei 10 : Vipeperushi vilivyotishia wahudumu wa afya wa Ebola katika maeneo ya Beni, Butembo na Oicha,vilisambazwa vikiwaambia waondoke maeneo hayo.
- Mei 13 : Vikosi vya usalama vilizima shambulio dhidi ya kituo cha matibabu ya wagonjwa wa Ebola cha Butembo, mshambuliaji aliuawa.
- Mei 13-14: Kituo cha afya cha Mutiri kilichopo eneo la Lubero kilivamiwa , vifaa vya matibabu vikaharibiwa na wahudumu wa afya wakatishiwa.
- Mei 17: Wahudumu wa mazishi ya heshmima na salama (EDS) walishambuliwa kwa matusi na wajumbe wa familia ya marehemu katika mji wa Bunia. Katika mji wa Butembo, wahudumu wa EDS walipigwa mawe.
- Mei 25 : Chumba cha vipimo vya awali katika kituo cha afya cha Vulamba mjini Butembo kilivamiwa na wezi waliopora vifaa. Katika kijiji cha Vusahiro katika kanda ya afya ya Mabalako, wakazi waliwavamia wahudumu wa afya, na kumuua mmoja wao.
- Juni 3: Vifaa viliibiwa kutoka katika maabara ya madibabu katika eneo la Komanda. Watu kumi wakauawa wakati wa uvamizi wa watu wenye silaha katika eneo la Rwangoma, mjini Beni, muda mfupi baada ya mazungumzo ya jamii yaliyoandaliwa na tiimu ya kukabiliana na Ebola.
- Juni 4 : Maandamano yalifanyika mjini Beni yalivuruga huduma za afya ya Ebola kwa umma.
- Juni 16 : Waendesha pikipiki na timu ya udhibiti wa maambukizi ya Ebola walikabiliana katika eneo la Rwampara, Ituri.
- Juni 17: Timu ya mazishi salama ya wagonjwa wa Ebola (EDS) ilishambuliwa mjini Bunia. Wahudumu wa timu hiyo walishambuliwa na kuibiwa.