Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Familia hazikuhudhuria mazishi ya wahanga wa ajali ya Ethiopian Airlines
Zipporah Kuria alikuwa akijaribu kujizuwia kutoa machozi.
Miezi minane baada ya ajali ya ndege ya Boeing 737 Max iliyomuua baba yake Zipporah Kuria , Joseph Waithaka, eneo la ajali lilifunikwa siku ya Alhamisi na mabaki ya miili ya wahanga wa ajali hiyo ambayo haikutambuliwa yalizikwa katika mageneza yanayofanana yaliyopangwa kwa mistari yalizikwa. Lakini Bi Kuria hakuwepo katika mazishi hayo.
Maafisa kutoka kampuni ya ndege ya Boeing na Ethiopian Airlines wanaaminiwa kuwa walihudhuria mazishi katika eneo la tukio , lakini kwasababu walichelewa kupata juu ya mazishi hayo Bi Kuria na ndugu wengine wa wahanga wa ajali hiyo hawakuweza kuhudhuria.
Jamaa wa wahanga wengine watatu tofauti wa ajali hiyo waliiambia BBC kuwa walifahamishwa kuhusu utaratibu huo wa mazishi siku mbili tu kabla ya tukio hilo. Matokeo yake , ni ndugu wawili tu wa wahanga 157 wa ajali ndio waliohudhuria.
"Ni upuuzi. Inanifanya nihisi mwili unatetemeka kutoka na huzuni kubwa ninapofikiria kwamba Boeing na Ethiopian Airlines wako katika mazishi ya baba yangu na mimi sipo ," Alisema Bi Kuria.
Ajali iliyokea katika eneo la kijijini Kusini-mashariki mwa mji mkuu wa Ethiopia, Addis Ababa. Iliacha shimo kubwa ambalo hadi kufikia wiki hii lilikuwa na vifusi na baadhi ya mabaki ya miili ya binadamu.
Familia za wale waliouawa zinasema kuwa zilijawa na uoga mkubwa baada ya kutembelea eneo la tukio mwezi uliopita na kubaini kuwa mvua za hivi karibuni zilizonyesha ziliacha mifupa ya miili ya wapendwa wao pamoja na vitu vingine nje baada ya kusoma udongo uliokuwa umeifunika. Baadhi wanasema mifupa ilikuwa inaelea kwenye maji ya mafuriko kndani ya shimo.
Ndege ya Ethiopian Airlines chapa ET302 ilipotea dakika chake baada ya kuondoka mjini Adis Ababa ikielekea katika mji mkuu wa Kenya Nairobi tarehe 10 Machi, 2019.
Ilianguaka katika ardhi ya shamba , katika eneo la kijiji. Mara baada ya ajali hiyo maiti ambazo zilibainika ziliondolewa , pamoja na visanduku vya kurekodi sauti ndani ya ndege na vifusi vikubwa vya ndege hiyo.
Unaweza pia kusoma:
Ajali inaaminiwa kutokea baada ya mfumo wa udhibiti wa ndege unaofahamika kama MCAS kutumiwa kwa wakati usiofaa, na hivyo kulazimisha pua ama sehemu ya mbele ya ndege kuelekea chini wakatti marubani walipokuwa wakijaribu kupaa juu zaidi.
Kasoro kama hiyo ilisababisha ajali ya ndege inayokaribia kufanana na hiyo chapa 737 Max nchini Indonesia mwaka uliopita. Ni miezi tisa sasa tangu ndege za Boeing zipigwe marufuku ya kusafiri na mamlaka za usafiri wa anga kote duniani.
Wakati mimi na wenzangu tulipotembelea eneo la ajali mwezi Mei , kulikuwa bado kuna vifusi vidogo vidogo vya ndege vilivyokuwa vimetapakaa ardhini.
Kulikuwa na shimo kubwa lililochimbika mahala ndege ilipoangukia pamoja na udongo mkubwa ulioachwa wakati waokoaji walipokuwa wakijaribu kufanya shughuli za uokozi , na uzio wa mbao ulikuwa ni kizuizi pekee cha kuzuwia watu kufika eneo la ajali hiyo. Hata hivyo wanyama waliweza kuzurura kwa uhuru katika eneo lote la tukio la ajali. Hapakuwa na walinzi wala afisa yeyote aliyewekwa eneo hilo.
Baada ya hayo, ndugu wa wahanga wanasema, hali ilikuwa mbaya zaidi kutokana na msimu wa mvua na wamekuwa wakitaka hatu ichukuliwa.
Nadia Millieron, ambae binti yake Samya Rose Stumo alikufa katika ajali hiyo , hivi karibuni aliiambia BBC kwamba : "Kulikuwa na mifupa iliyokuwa ikifichuliwa na mahi ya mafuriko kila wakati na wenyeji walikuwa wakienda kwenye eneo la ajali na kuifunika . Tunataka Ethiopian Airlines kumwaga rundo la udongo kwenye shimo na ichukue masalia ya miilio ambayo haijatambuliwa ndani ya shimo na ifunike kila kitu ".
Ethiopian Airlines, ambayo ndiyo inayosimamia eneo la ajali , iiliziambia familia za ''waathiriwa'' wa mkasa huo kuwa inaelewa tatizo , lakini ikadai kuwa masuala ya bima yameizuwia kuchukua hatua . Lakini baada ya kukabiliwa na shinikizo kutoka kwa ndugu wa marehemu, na kufuatia uchunguzi wa BBC, inaonekana matatizo hayo sasa yametatuliwa.
Alhamisi, mistari ya majeneza ulipangwa vizuri katika shimo ilikoangukia ndege . Majeneza hayo yalikuwa na masalia ya miili ambayo awali yalitolewa kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi lakini hayakuweza kubainika baada ya kuharibika . Baada ya kuwekwa kwenye shimo hilo yalifunikwa na shimo likafunikwa kwa udongo uliolundikwa wakati wa shughuli za uokozi.
Eneo la ajali hiyo sasa ni kaburi la kudumu.
Ndugu wa waahanga wa ajli wanaamini Ethiopian Airlines ilikuwa na wajibu wa kuwafahamisha juu ya mazishi na ingewapatia taarifa zaidi. BBC iliwasiliana na kampuni hiyo ya ndege kutaka kauli yake.
Boeing imekataa kutoa kauli juu ya ripoti kwamba mmoja wa maafisa wake wa ngazi ya juu, Jennifer Lowe, alikuwa ni mmoja wa watu waliohudhuria mazishi.
Kampuni hiyo ilisema kuwa katika kauli yake : "Tunaendelea kutoa rambirambi zetu kwa familia na wapendwa wa wahanga wa ajali ya Ethiopian Airlines chapa 302 na Lion Air chapa 610 na tuko tayari kuwasaidia wale walioathiriwa na mikasa hii ."
Mwezi uliopita Bi Kuria alisafiri na familia yake hadi Ethiopia kukusanya na kuleta baadhi ya masalia ya mwili wa baba yake. Alisema ilikuwa ni "jambo la kuvunja moyo " kwamba hakuweza kufika katika eneo la ajali wakati shimo lilipokuwa linafunikwa katika eneo la ajali.
"Baba yangu anazikwa , sehemu kubwa ya mwili wake, wakati sisi tulipewa sehemu yake ndogo turudi nayo ," alisema
Alisema kuwa angeirikuia ndege na kusafiri kama ingewezekana.
"Walitunyima fursa ya kuzika ," alisema.