Je ni wanaume gani katika hatari ya kupata tezi dume?

Man in medical appointment

Chanzo cha picha, Getty Images

Wataalamu wanasema kuwa wanaume wanaozaliwa na hatari ya kupata tezi dume wanatakiwa wawe na vipimo vya mara kwa mara katika kipindi cha mwaka mzima kuanzia miaka 40.

Wanaume wenye aina fulani ya mabadiliko kwenye vinasaba vyao wana uwezekano zaidi wa kupata tezi dume.

Wanasayansi katika kituo cha utafiti cha magonjwa ya saratani (ICR) wanasema kuwa vipimo vya awali kabisa vya damu vinaweza kusaidia kujulikana kwa uvimbe mapema zaidi, na ni rahisi pia kutibu.

Lakini wengi hawawezi kujua kama wana mabadiliko katika vinasaba na gini zao kutokana na vipimo hivyo hufanywa mara chache.

Unaweza pia kusoma:

Idara ya saratani ya tezi dume Uingereza wamesema kuwa uamuzi wowote unahitajika kufanywa kwa tahadhari.

Watafiti wa ICR wanasema kuwa katika wanaume 300 huko Uingereza, mmoja ana mabadiliko katika vinasaba na gini zake ambapo anakuwa na hatari zaidi ya kupata tezi dume.

tezi dume
Maelezo ya picha, saratani ya tezi dume

Mabadiliko ya vinasaba ni sawa kabisa na matatizo ya gini ambayo kwa wanawake husababisha saratani ya matiti pamoja na ya kizazi, kwa wanaume atapata pale ambao itakuwepo katika familia yao.

jinsi ya upimaji

Tezi dume hupimwa kwa kupitia protini ambazo zinatengenezwa kwenye sehemu ya uzazi ya mwanaume (prostate gland)

Protini hizo zikiongezeka basi inawezekana itakuwepo tezi dume, lakini si kipimo cha uhakika cha kuthibitisha uwepo wa ugonjwa.

Unaweza pia kusoma:

Profesa wa Ros Eeles anasema kuwa ''tafiti yetu inaonesha kuwa wanaume wenye matatizo kwenye gini na vinasaba wana uwezekano mkubwa wa kupata tezi dume na kutumia vipimo hivi kunaweza kusababisha wapate matibabu ya haraka na mapema zaidi.

Profesa Eeles amekua akiibua suala hili kwa muda mrefu katika mkutano wa vituo vya utafiti wa saratani huko Glasgow.

Utafiti mwingine uliofanywa ulionesha wanaume wenye viuno vikubwa wana hatari ya kupata saratani ya tezi dume.

Utafiti uliofanyiwa watu 140,000 kutoka mataifa manane ya Ulaya ulibaini kwamba viuno vikubwa huongeza mtu kupatikana na saratani hiyo kwa asilimia 13.

Wanaume ndio waliomo hatarini zaidi wakiwa na ukubwa wa nchi 37 ,kulingana na utafiti huo wa chuo kikuu cha Oxford.

Unaweza pia kutazama

Maelezo ya video, Ayalo: Nimeumizwa sana na saratani ya tezi dume

Saratani ya tezi dume ndio ilio na visa vingi miongoni mwa wanaume.