Watanzania wasema nini juu ya uamuzi wa mahakama kuzuwia ndoa za wasichana wadogo?

Chanzo cha picha, Getty Images
- Author, Na Dinah Gahamanyi
- Nafasi, BBC News Swahili
- Muda wa kusoma: Dakika 2
Mahakama ya juu zaidi Tanzania imebatilisha sheria inayoruhusu familia kuwaoza wasichana wadogo wenye umri wa kuanzia miaka 14.
Mahakama kuu ya rufaa imebatilisha uamuzi uliotolewa awali na mahakama nyingine nchini kwa misingi ya kuwa ndoa za watoto zinakiuka haki za wasichana, na nii kinyume cha sheria na katiba ya nchi hiyo.
Unaweza pia kusoma:
Mwanasheria mkuu wa Tanzania alikuwa amekata rufaa juu ya uamuzi wa mahakama ya juu wa mwaka 2017, ambapo ilikuwa imeondoa vipengele vya sheria na kuruhusu ndoa kwa wasichana wenye umri wa kuanzia miaka 14.

Mahakama hii leo ilisema kuwa wasichana hawawezi kuolewa kabla ya kutimiza umri wa miaka 18, umri ambao wavulana pia wanaruhusiwa kuoa.
Uamuzi huu wa mahakama ni hatua iliyopigwa katika kutetea haki za wasichana. Taarifa ya kuzuiwa ndoa za mapema kwa wasichana imepokelewa kwa hisia mbali mbali katika mitandao ya kijamii.
Shirika la Msichana Initiative ambalo ndilo lililowasilisha kesi mahakamani kupinga sheria ya kuolewa kwa wasichana wadogo, limesema: ''Maamuzi ya leo ni maamuzi muhimu kwa wasichana wa leo na wa baadae.
Kwetu sisi kama shirika na kupitia mawakili wetu, tunaona huu ni uamuzi sahihi kwasababu unaendana na kasi ya maendeleo ya taifa hili katika kuwalinda watoto wa kike'' amesema Rebecca Byumi afisa mkuu mtendaji wa shirika hilo.
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe, 1

Mwisho wa X ujumbe, 2
Shirika la Gender TZ limeelezea kwamba sheria iliyokuwepo iliwanyanyasa sana vijana hasa wa vijijini:
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe, 3

Mwisho wa X ujumbe, 4
Unaweza pia kusoma:
Kwa mujibu wa shrika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia masuala ya watoto Unicef, 31% ya wasichana nchini Tanzania huolewa kabla ya kutimiza umri wa miaka 18, huku 5% wakiolewa kabla ya kustimiza miaka 15.
Unaweza pia kutazama: