Wanawake 100 wa BBC 2019: Tanzania, Kenya, DR Congo, Uganda, Somalia, ni nani aliyemo kwenye orodha mwaka huu?

BBC imetangaza orodha ya wanawake 100 walio na ushawishi kutoka kote duniani 2019.

Mwaka huu BBC 100 Women inauliza: Mustakabali umekaaje iwapo utaendeshwa na wanawake?

Kuanzia msanifu mijengo anayepanga kuijenga upya Syria, hadi msimamizi kutoka shirika la anga za juu Nasa , wa mradi wa helikopta itakayoruka katika sayari ya Mars - wengi katika orodha hii wamebobea katika nyanja tofuati wanazowakilisha na wanatupatia tathmini ya jinsi maisha yatakavyokuwa kufikia 2030.

Wengine kama mwanasiasa "pepo" anayekiuka kundi la mafia, na wachezaji soka wanaopambana na chuki dhidi ya wanawake, wanatumia vipaji na uzoefu wao kuunda njia kwa vizazi vinavyofuata.

Wanawake 100 wa BBC 2019 wameorodheshwa kwa herufi za majina yao, kazi zao, mataifa wanayotokapamoja na wasifu wao .

Wanawake wa kutambulika Afrika:

81) Nanjira Sambuli - Mtaalamu wa kidijitali, Kenya

Nanjira anaongoza shirika la World Wide Web Foundation katika jitihada zake za kuongeza usawa katika masuala ya kidijitali.

Anatafuta suluhu kuhakikisha hakuna anayeachwa nyuma linapokuja suala la kufikia mtandao, ima ni wasiojiweza au kwa utofauti wa kijinsia lakini pia kijiografia.

63) Benedicte Mundele - Mfanyabiashara wa vyakula vya kutoka shambani, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo

Benedicte akiwa na miaka 24, alitazama ndani ya nchi ya Congo akaona kuna vyakula vingi vya kutoka shambani kama viazi, na matunda ya passion, lakini watu bado wanaishi kwa umaskini wa chakula.Anasema maduka makubwa yanauza bidhaa ambazo zilikuzwa DRC lakini zilizosafirishwa nje zikihifadhiwa kwa madawa kabla ya kuingizwa tena nchini na kuuzwa kwa gharama kubwa. Katika kukabiliana na hilo, aliidhinisha Surprise Tropical, duka la kuuza vyakula vyenye afya zikiwemo sharubeti na ndizi za mkono wa tembo katika mitaa ya mji mkuu Kinshasa. Miaka mitano baadaye kampuni yake imeimarika katika mtandao na husambaza vyakula vya shambani kote mjini huku akiwana mipango ya kuipanua biashara kote katika Jamhuri ya Kidmeokrasi ya Congo.

16) Judith Bakirya - Mkulima, Uganda

Judith Bakirya amelelewa shambani nchini Uganda. Alikuwa wa kwanza miongoni mwa vijana wenzake kushinda ufadhili kwenda shule tajika ya wasichana ya malazi na kufanikiwa kupata shahada ya uzamifu nchini Uingereza na hatimaye kuajiriwa mjini huko.

Lakini hakuridhika na kazi yake, na akatumia akiba ya fedha alizokuwa nazo kurudi nyumbani na kuidhinisha shmba la kukuza matunda, Busaino Fruits & Herbs. Tangu kushinda tuzo ya ukulima , ametumia jukwa ahili kuangazia haki za wanawake, ikiwemo kunyimwa umiliki wa ardhi, kukosa elimu na unyanyasaji wa nyumbani dhidi yao.

79) Jawahir Roble - Refa katika soka, Uingereza/Somalia

Jawahir Roble ni mwanamke wa kwanza nchini Uingereza mwenye aisli ya Kisomali , anayevaa hijab katika kazi yake ya urefa kwenye soka. Aliwasili Uingereza akiwnaa umri wa miaka 10, aligundua anapenda michezo hatua iliyomuongoza na kuwa refa. Anasomea ukufunzi na usimamizi wa soka, akitarajia kukamilisha shahada yake mwaka 2020.

45) Gada Kadoda- Mhandisi, Sudan

Dkt Gada Kadoda huwasaidia wanawake katika maenoe ya mashambani kutumia nishati ya jua kupata umeme vijiini kwa kuwafunza kuwa wahandisi wa kijamii. Alitajwa kuwa mvumbuzi wa Unicef wa kutazamiwa katika siku za usoni kama kiungo kikuu cha kuidhinishwa maabara ya kwanza ya uvumbuzi Sudan, inayowapatia wanafunzi nafasi ya kushirikiana na kutatua matatizo. Ni muasisi wa Sudanese Knowledge Society, inayowapa fursa watafiti vijana kuwasiliana wazi na wanasayansi na wasomi ndani na nje ya nchi.

47) Ahlam Khudr - Kiongozi wa maandamano, Sudan

Amejitangaza kuwa 'mama wa mashahidi wote Sudan', mtoto wake wa kiume Ahlam aliye na miaka 17 aliuawa katika maandamano ya amani mnamo 2013. Tangu hapo Ahlam amejitolea maisha yake kuitisha haki kwa niaba yake na kupigania haki za waliouawa au 'kutoweka' nchini Sudan. Alikuwa sehemu ya majukwaa ya chini kwa chini na maandamano na "alipigwa vibaya" alipokamatwa na vikosi vya usalama. Katika vuguvugu hilo lililoanza mnamo Desemba 2018 dhidi ya wakati huo - Rais Omar al-Bashir, Ahlam alikuwa mwandamanaji maarufu, aliyeongoza mikutano iliyokuwana ufuasi mkubwa wa vijana.

90) Kalista Sy - Muandishi na mzalishaji vipindi, Senegal

Kalista Sy alijifunza mwenyewe uandishi wa vipindi na makala yake katika Televisheni 'Mistress of a Married Man' ilitiisa nchini mwake ilipozinduliwa mwaka huu. Inaangazia wanawake walio huru katika mahusiano, wanaofanya kazi kwa bidii na waliofanikiwa wanaoangazia jitihada za wanawake wa Afrika magharibi, katika suala la ndoa za wake wengi hadi pia masuala ya unyanyasaji wa ndani ya nyumba na masuala ya afya ya akili.

30) Lucinda Evans - Mwanaharakati wa kutetea haki za wanawake, Afrika kusini

wakati Afrika kusini inakabiliwa na visa vinavyoongezeka vya mauaji na ubakaji dhidi ya wanawake na wasichana, Lucinda amekuwa suati ya wanawake. Yeye huongoza maandamano ya kitaifa, kuwashinikiza maelfu ya wanawake katika mji wa Cape Town, na kuishinikiza serikali ichukue hatua na sio kuidhinisha sera tu. Lucinda aliidhinisha shirika lisilo la serikali - Philisa Abafazi Bethu (waponye wanawake wetu), linalotoa huduma zikiwemo ushauri nasaha, kusaka wasichana waliotekwa katika jamii na kuwapa hifadhi salama wanawake waliokabiliwa na unyanyasaji wa nyumbani.

42) Asmaa James- Mwandishi habari/mwanaharakati, Sierra Leone

Kupitia uandishi habari na shughuli katika jamii, Asmaa amekuwa sauti ya wasio na suati nchini.

Baada ya kusikia kuhusu ubakaji wa msichana wa miaka mitano, alitumia jukwaa lake katika mtandao wa kijamii kuidhinisha kampeni iliyowahimiza wanawake kuvaa nguo nyeusi kila Jumanne ya kila mwezi kulalamika khusu ongezeko la visa vya ubakaji na unyanysaji wa wasichana wa chini ya miaka 12. Kampeni hiyo kwa jina Black Tuesday - ilichangia hatua kutoka kwa serikali kufanya mageuzi ya sera za unyanyasaji wa kingono nchini.

69) Farida Osman - Muogeleaji, Misri.

Alipewa jina 'samaki wa dhahabu', mnamo 2017 Farida aliibuka mwanamke wa kwanza nchini Misri kushinda medai alipopokea medali ya shaba katika mashindano ya 50m mtindo wa butterfly katika mashindano ya ubingwa ya majini - FINA. Ameshinda shaba nyingine mwaka huu. Yeye hutoa mihadhara katika vyuo vikuu kuwatia moyo vijana kuingia katika uogeleaji, na anapokea mafunzo kutimiza ndogo yake ya kushinda medali katika mahsindano ya Olimpiki nchini Tokyo 2020.

61) Raja Meziane - Muimbaji, Algeria

Video ya musiki wa kisiasa ya Raja Meziane Allo le Système! Imetazamwa mara milioni 35 katika mtanao wa YouTube. Nyimbo zake dhidi ya serikali zinakabiliana na ukosefu wa usawa katika jamii, tuhuma za ufisadi na ukosefu wa usawa - ambazo zimemlazimisha kuishi uhamishoni nje ya Algeria. Anaishi Prague hivi sasa, na yeye anaunga wazi mkono maandamani nchini Algeria mwaka huu yaliochangia maelfu ya vijana kushuka barabarani kuitisha mageuzi.

9) Rida Al Tubuly - Mwanaharakati anayeshinikiza amani, Libya

Rida Al Tubuly ni mojawapo ya wanawake wengi wanaoshinikiza usawa wa kijinsia - lakini analitekeleza hilo kutoka eneo linalokumbwa na vita. Shirika lake - Together We Build It, linashinikiza kuhusika kwa wanawake katika kuutatua mzozo nchini Libya.

Wengine kwenye orodha ya wanawake bora 100 wa BBC 2019:

1) Precious Adams- Mcheza Ballet, Marekani

Akiwa na miaka 8, Precious Adams alitumia muda mwingi kucheza dnasi nyumbani na mamake akamsajili kwa mafunzo ya kudansi. Alipotimia miaka 16 , alishinda nafasi katika shule tatu maarufu duniani za Ballet ikiwemo ya Bolshoi Ballet Academy Urusi.

2) Parveena Ahanger - mwanaharakati wa haki za binaadamu, Kashmiri inayoongozwa na India

Parveena anafahamika kama 'mwanamke chuma wa Kashmir'. Mwanawe alipotea mnamo 1990, wakati wa vuguvugu dhidi ya utawala wa India Kashmir.

3) Piera Aiello - Mwanasiasa, Italia

Anafahamika kama mwanasiasa "pepo" Piera Aiello aligombea wadhifa akiwa amejifunika uso kutokana na tishio kutoka kwa mafia. Mwaka jana, baadaya kushinda kiti kama mgombea anayepinga mafia, hatimaye aliufunua uso wake hadharani.

4) Jasmin Akter - Mcheza kriketi, Uingereza/Bangladesh

Jasmin anatoka katika jamii ya Rohingya, inayotaja na Umoja wa mataifa kamakundi la wachache linalokabiliwana maovu duniani. Alizaliwa katika kambi ya wakimbizi Bangladesh muda mfupi baada ya babake kufariki.

5) Manal AlDowayan - Msanii, Saudi Arabia

Sanaa ya Manal AlDowayan inagusia kutoonekana, hifadhi za kale, kumbukumbu na uwakilishi wa wanawake nchini mwake.

6) Kimia Alizadeh - Mpiganaji Taekwondo, Iran

Mnamo 2016, Kimia alikuwa mwanamke wa kwanza nchini Iran kushinda medali katika Olimpiki tangu taifa hili lianze kushiriki mashindano mnamo 1948. Kama mwanariadha wa taekwondo, Kimia anasifika na gazei la Uingereza Financial Times kwa "kuwaimarisha wanawake na wasichana nchini Iran kuvuka mipaka iliyowekwa ya uhuru binafsi".

7) Marwa Al-Sabouni- Manifu mijengo, Syria

Wakati vita vilipozuka nyumbani alikozaliwa msanifu mijengo Marwa Al-Sabouni katika mji wa Homs, nchini Syria, alikataa kuondoka.

Ameandika kitabu kunakili muda huo wote, na amechora ramani za kuijenga upya wilaya iliyoharibiwa ya Baba Amr katika namna ambayo itajumuisha watu wa tabaka na makabila mbali mbali pamoja.

8) Alanoud Alsharekh - Mwanaharakati wa haki za binaadamu, Kuwait

Dkt Alanoud Alsharekh ini miongoni mwa wafuasi wa kwanza wa kampeni ya 'Abolish 153 ', iliyoshinikiza kufutiliwa mbali kwa mauaji ya kutunza heshima Kuwait. Anashirikiana na mashirika kuimarisha usawa wa kijinsia mashariki ya kati.

10) Tabata Amaral - Mwanasiasa, Brazil

Tabata Amaral, mojawapo ya wabunge vijana Brazil, alimulikwa kitaifa mwaka huu wakati video yake aliyoonekana akimhoji waziri wa fedha iliposambaa mitandaoani. Kama mbunge, ajenda yake kuu ni elimu haki za wanawake, uvumbuzi wa kisiasa na mustakabali endelevu.

Kwa mtiririko:

11) Yalitza Aparicio - Actress and human rights activist, Mexico

12) Dayna Ash - Cultural activist, Lebanon

13) Dina Asher-Smith - Athlete, UK

14) MiMi Aung - Project manager at Nasa, US

15) Nisha Ayub - Transgender rights activist, Malaysia

17) Ayah Bdeir - Entrepreneur, Lebanon

18) Dhammananda Bhikkhuni - Monk, Thailand

19) Mabel Bianco - Doctor, Argentina

20) Raya Bidshahri - Educator, Iran

21) Katie Bouman - Scientist, US

22)Sinead Burke - Disability activist, Ireland

23) Lisa Campo-Engelstein - Bioethicist, US

24) Scarlett Curtis - Writer and campaigner, UK

25) Ella Daish - Environmentalist, UK

26) Sharan Dhaliwal - Writer and artist, UK

27) Salwa Eid Naser - Athlete, Nigeria/Bahrain

28) Rana el Kaliouby- Artificial intelligence pioneer, Egypt

29) Maria Fernanda Espinosa - President of UN General Assembly, Ecuador

31) Sister Gerard Fernandez- Roman Catholic nun, Singapore

32) Bethany Firth - Paralympic swimmer, UK

33) Owl Fisher - Journalist and trans rights campaigner, Iceland

34) Shelly-Ann Fraser-Pryce - Athlete, Jamaica

35) Zarifa Ghafari - Mayor, Afghanistan

36) Jalila Haider - Lawyer, Pakistan

37) Tayla Harris - Australian rules footballer and boxer, Australia

38) Hollie - Trafficking survivor, US

39) Huang Wensi- Professional boxer, China

40) Luchita Hurtado - Artist, Venezuela

41) Yumi Ishikawa - Founder of the #kutoo movement, Japan

42) Asmaa James- Journalist/activist, Sierra Leone

43) Aranya Johar - Poet, India

44) Katrina Johnston-Zimmerman - Anthropologist, US

45) Gada Kadoda- Engineer, Sudan

46) Amy Karle - Bioartist, US

47) Ahlam Khudr - Protest leader, Sudan

48) Fiona Kolbinger - Cyclist, Germany

49) Hiyori Kon - Sumo wrestler, Japan

50) Aïssata Lam - Microfinance expert, Mauritania

Picha kwa hisani: Hakimiliki ya picha: Karolina Kuras, Hans Jørgen Brun, Nicola Virzì, Sage Sohier, Christian Petersen/Getty Images, Mooreyameen Mohamad, Amelia Allen, Getty Images/Maja Hitij, UN, British Swimming, Hauser & Wirth, Oresti, Tsonopoulos, Kawori Inbe, Amal Adam, Matt Kay, Constanza Lavagna, Paula Mitre, Theo Kruse, Venura Chandramalitha, Luis Crispino/Claudia Magazine, Anders Hellberg, Graciela Buffanti, Wakophotography, IBF China, Germana Costanza Lavagna, Neal Hardie, Sharon Kilgannon, Hanna Sotelo, Sumit Kumar Singh, Päivi Mäkelä, Pimienta Films, Siddharth Das, Venura Chandramalitha, Linda Roy by Irevaphotography

Je wanawake 100 ni nini?

BBC 100 Women huwataja wanawake 100 wenye ushawishi na wenye kutia moyo kote duniani kila mwaka na tunaangazia hadithi zao.

Mwaka huu, BBC 100 Women inauliza: Mustakabali umekaaje iwapo utaendeshwa na wanawake?

Jumuika nasi kwenye Facebook, Instagram na Twitter na tumia #100Women