Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Robert Mugabe: Wazimbabwe wamkumbuka 'mkombozi na mkandamizaji'
Maoni mgawanyiko yaliyotolewa kumuhus Robert Mugabe alipokuwa hai, hayabadilika hata baada ya mauti yake . Wazimbabwe wanakumbuka kuhusu ni nini alichowaachia kiongozi huyo aliyeiongoza Zimbabwe kwa miaka 37.
Wakitumia #RIPMugabe ama #LALAsalama baadhi wanamsifu ama shujaa, mtetezi wa hadi ya watu weusi, huku wengine wakisema alikuwa mkombozi aliyegeuka kuwa mkandamizaji . Wakili wa Zimbabwe , mwanaharakati na mkosoaji wa serikali ya chama cha Zanu-PF , Fadzayi Mahere, anatafakari maoni tofauti kumuhusu namna Bwana Mugabe atakavyokumbukwa:
Baadhi ya jumbe za Twitter zilizolenga namna Mugabe atakavyokumbukwa kwa uchumi wake ambao uliathiri kila sekta ya maisha , hususan huduma za matibabu
Hospitali za umma zimetawaliwa na ufisadi pamoja na usimamizi mbaya , hali ambayo imesababisha utoaji wa huduma duni kwa wa wagonjwa.
Madaktari na wauguzi hufanya migomo ya mara kwa mara kuhusu mishahara .
Kwamba Bwana Mugabe - Mpigania haki za Waafrika aliyekuwa mstari wa mbele - mara kwa mara amekuwa akipata matibabu nchini Singapore na amefariki katika nchi ya kigeni ni kitu ambacho hakitasahaulika miongoni mwa wengi.
Baadhi ya Wazimbabwe pia wanatafakari juu ya kile ambacho kingetokea
Bwana Mugabe alichukua uongozi wa kitaifa akitoa ahadi nyingi nzuri mwaka 1980 alipokuwa Waziri Mkuu wa kwanza. Awali katika kazi yake ya kuleta maridhiano na kuiendeleza Zimbabwe, lakini kazi yak yote nzuri iliharibika alipoanza kampeni ya kuwatesa wwapinzani na kujilimbikizia mali binafsi na familia yake
Kwa baadhi hata hivyo, hakuna kitu kitakachoindoa thamani yamazuri aliyoyaacha Bwana Mugabe na kwamba atakumbukwa kama nmkombozi dhidi ya mamlaka ya wakoloni na seikali za magharibi