Mat Dan: ' Adai kupata umaarufu bila kutegemea maili 6000 kutoka nchini mwake

A poster for one of Dan's shows

Chanzo cha picha, Mat Dan

Maelezo ya picha, Tangazo la picha linalomuonyesha Mat Dan

Mohammed Kareef Daniel Abdullah anapowasili katika mji mkuu wa Malaysia, haichukui muda mrefu kabla ya watu kuanza kumshangilia kwa shangwe.

" Watu umshangilia na kumuita Mat Dan kwa kelele na kumuomba kupiga picha!'" mama yake aeleza.

Kuna wale ambao wamemsikia katika kipindi cha asubuhi cha redio au kumuona katika tangazo la picha barabarani akiwa anatangaza safari za utalii, mjini Mecca. Mat Dan ni habari kubwa Malaysia.

Short presentational grey line

Jinsi Dan alivyokuwa katika maisha yake ya hali ya kati, umaarufu anaoupata ni jambo kubwa sana kwake na sio kitu cha kawaida.

Dan during a holiday to Magaluf in 2007

Chanzo cha picha, Alex Duncan

Mwaka 2008, Dan alitunza fedha kiasi na kuamua kwenda mapumzikoni kusini mashariki mwa Asia akiwa na marafiki zake.

Licha ya kwamba alirudi Uingereza baada ya miezi kadhaa, aliamua kurudi katika bara hilo mwaka huo huo.

Hakujua hata kidogo kuwa kurejea kwake katika eneo hilo kungeweza kubadili maisha yake.

Dan aliamua kujichanganya na watu wa fukwe hizo na wakati alipokuwa anajaribu kutamka baadhi ya maneno ya eneo hilo kwa kukosea, alirekodiwa na mwanafunzi wa Kuala Lumpur bila kujijua.

Short presentational grey line

Mwanafunzi huyo aliyemrekodi Dan kwa siri, aliweka video hiyo kwenye mtandao wa Youtube na maelfu ya watu waliweza kujiona.

Televisheni zilimtafuta wakimtaka Dan kutangaza na kumpa muda mzuri wa matangazo.

During filming of 'Haramain Backpackers - Trans Siberian'

Chanzo cha picha, Mat Dan

Mara ya kwanza, kipindi chake kiliporuka hewani, maisha yake yalibadilika ndani ya usiku mmoja tu.Alipata wafuasi zaidi ya laki nane katika mtandao wa Instagram.

Kipindi cha pili, alitengeneza mfululizo wa namna ambavyo alikuwa anajua kupika wakati hajui kupika.

Baadae alianzisha kipindi cha redio nchini humo kwa kuwasiliana wasikilizaji.

"Kila duka , kila mgahawa, kila barabara ninayopita ninaitwa'Hey Mat Dan, Mat Dan!', hivyo amebakia kuwa mtu wa kupiga picha na watu asiowajua," rafiki yake Dan aliyemtembelea mwaka 2017.

Kwa sasa ueleo wake wa lugha na tamaduni ya Malaysia inamfanya kuwa mtu wa kipekee katika eneo hili.

Dan with his wife and child in Mecca

Chanzo cha picha, Mat Dan

Maelezo ya picha, Dan akiwa na mke wake, Nurnadifa, na mtoto wao Zayne wakiwa Makka

Dan alibadili dini na kuwa muislamu ili kumuoa mke wake Nurnadifa.

Anasema hawezi kukubali kufanya kazi ambayo itaenda kinyume na maadili ya dini yake, mfano kutangaza tangazo la pombe au kumuonyesha mapenzi mtu mwingine.

Pamoja na kwamba wengi wanapenda matangazo yake barabarani, wapo pia ambao wanakosoa utendaji wake wa kazi.

Na Dan anasema anaheshimu uhuru wa maoni ya kila mmoja.

Short presentational grey line

Licha ya kwamba Dan anaishi Malaysia kwa sasa, bado anaenda Uingereza mara kwa mara kuona ndugu zake.

Dan's mum, Nicola, and dad, Kevin, with Nurnadifa and Zayne

Chanzo cha picha, Mat Dan

Maelezo ya picha, Wazazi wa Dan, mke wake Nurnadifa na Zayne

Familia yake inafurahia umaarufu ambao Dan ameupata nje ya nchi , pamoja na mabadiliko mengi aliyoyafanya katika maisha yake, wanaamini kwao bado ni Dan yule yule.

"

Short presentational grey line
Dan is now a tourism ambassador for Terengganu state

Chanzo cha picha, Mat Dan

Maelezo ya picha, Dan ni balozi wa jimbo la utalii la Terengganu

" Ninajiona kuwa ni Mmalesia zaidi ya muingereza." Dan alisisitiza