Profesa Kabudi akanusha kuthibitisha 'kifo' cha Azory Gwanda

Gwanda

Chanzo cha picha, HRW

Maelezo ya picha, Azory Gwanda kabla ya kutoweka kusikojulikana
Muda wa kusoma: Dakika 2

Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania, Profesa Palamagamba Kabudi amekanusha kuwa amethibitisha 'kifo' cha mwanahabari Azory Gwanda.

Msemaji mkuu wa serikali ya Tanzania, Dkt Hassan Abbas amemnukuu Proefa Kabudi kwa kupitia mtandao wake wa kijamii wa Twitter akisema: "Nimepokea kwa masikitiko taarifa potofu zinazoendelea kuchapishwa kwenye mitandao ya kijamii ikinukuu kimakosa mahojiano yangu kwenye kipindi cha BBC FOCUS ON AFRICA zikidai kuwa nimethibitisha kwamba mwanahabari Azory Gwanda amefariki dunia."

Lakini Prof Kabudi pia amesema bado haijulikani kama Bw Gwanda yungali hai: "Mpaka sasa hakuna uthibitisho kuwa Azory yuko hai au amefariki. Vyombo vya ulinzi na usalama vinaendelea kuchunguza tukio hilo na matukio mengine yaliyotokea katika machafuko ya Kibiti, Pwani yaliyosababisha ama watu kadhaa kupoteza maisha au kupotea."

Kabudi amesema kuwa, kilichotokea ni tafsiri potofu ya kile alishokisema: "Hii sio tafsiri sahihi kuhusu kile nilichokisema. Katika mahojiano hayo nilieleza kuwa tukio lililotokea Kibiti lilikuwa ni la kuhuzunisha na wapo watanzania waliouwawa na wengine kupotea. SIKUTHIBITISHA kuwa Azory Gwanda amefariki."

Ruka X ujumbe
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: Imetoka kwingine na inaweza kuwa na matangazo

Mwisho wa X ujumbe

Katika mahojiano hayo ambayo yalirushwa jana Alhamisi Julai 10, 2019 Profesa Kabudi alisema kwa kingereza kuwa mwandishi huyo "...has disappeared and died" ikiwa na maana kuwa 'alitoweka na kufariki'.

"...Azory Gwanda ni sehemu ya Watanzania wengine wengi ambao wameuawa katika eneo lile (kibiti)," alisema Kabudi na kusisitiza kuwa yaliyotokea Kibiti na Rufiji ilikuwa ni kipindi cha uchungu zaidi katika historia ya Tanzania.

''Wacha nikwambie unapozungumzia kuhusu kisa hicho, ni mojawapo ya visa ambavyo vimesababisha uchungu mwingi nchini Tanzania,'' alisistiza Prof Kabudi.

pROFESA kABUDI
Maelezo ya picha, Profesa Kabudi akiwa anahojiwa na BBC

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa awali na kampuni ya magazeti ya mwananchi, mwanahabari huyo wa kujitegemea alitoweka tarehe 21 Novemba.

Bw Gwanda alikuwa anaishi na kuripoti kutoka mji mdogo uitwao Kibiti, ambao upo kilomita kama 130 hivi kusini mwa Dar es Salaam.

Alikuwa ni mmoja wa waaandishi wa kwanza kabisa kuripoti kwa kina juu ya mfululizo wa mauwaji yaliyokuwa yakitekelezwa na watu wasiojulikana yaliyowalenga polisi na viongozi wa mji huo.

Mke wake Anna Pinoni alisema watu wapatao wanne wakiwa kwenye gari aina ya Toyota Land Cruiser nyeupe walimchukua bwana Gwanda kutoka katikati ya mji huo, mahali ambapo hupendelea kukaa.

Anasema pia aliporudi nyumbani alikuta vitu vimezagaa, ishara kwamba inawezekana waliipekua nyumba yao.

Bw Azory aliwasiliana na ofisi za Mwananchi mara ya mwisho tarehe 20 Novemba kwa majukumu ya kikazi.

Anadaiwa kutekwa katika operesheni iliofanyika katika pwani ya wilaya ya Kibiti ambapo mauaji ya kiholela yalikuwa yakifanyika.