Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Jaguar: Mbunge wa Kenya aliyetoa kauli za chuki kusalia rumande
Mbunge wa Kenya Charles Njagua Kanyi maarufu Jaguar ataendelea kuzuiliwa katika kituo cha polisi kwa siku zingine nne baada ya mahakama kumnyimwa dhamana.
Jaguar alikamatwa nje ya bunge la Kenya siku ya Jumatano na kufikishwa mahakamani siku iliyofuatia.
Mahakama imewapatia polisi siku tatu zaidi kuendelea na uchunguzi dhidi ya kauli za kichochezi dhidi ya wafanyabiashara wa kigeni katika soko kuu la Gikomba nchini Kenya.
Alipokuwa akizungumza kuhusu kuwepo kwa ushindani wa kibiashara na wageni usio na usawa, alisema: ''Wakenya ni sharti wafanye biashara zao bila kushindana na watu kutoka mataifa mengine.Raia wa China wametawala biashara za kuuza magari nchini humu, Watanzania na Waganda wanatawala katika masoko yetu. Tunasema imetosha iwapo hawatarajeshwa nyumbani katika saa 24 tutawashika na kuwapiga na hatuogopi mtu yeyote'', alinukuliwa akisema.
Kauli hiyo iliibua hisia kali kwenye mitandao ya kijamii.Hisia tofauti zimeibuka kufuatia matamshi aliyotoa mbunge wa Kenya dhidi ya wachuuzi wa kigeni wanaoendehsa biashara nchini Kenya.
Katika kanda ya video iliosambazwa nchini Kenya na katika nchi jirani Tanzania, mbunge huyo Charles Njagua Kanyi, alisema hawatokubali watu wa nje waje kuendesha biashara nchini.
"...Ukiangalia soko zetu, Watanzania na Waganda wamechukua biashara zetu, sasa sisi tumesema enough is enough".
Mbunge huyo hata hivyo amesema kuwa kauli yake ''ilitafsiriwa'' visivyo.
Jaguar ni nani?
Charles Njagua Kanyi al maarufu Jaguar ni mwanamuziki, mwanasiasa na mjasiliamali na inaaminiwa kuwa mmoja wa wasanii tajiri nchini Kenya na katika eneo la Afrika Mashariki
Alizaliwa katika familia ya maskini katika familia ya watoto watatu. Jaguar alisomea katika shule ya msingi mjini Nairobi na akiwa na umri wa miaka 11 alifiwa na mama yake ambaye wakati huo alikuwa ndiye mlezi wake pekee.
Alilazimika kufanya kazi za vibarua ili kujikimu kimaisha na moja ya kazi alizozifanya ilikuwa ni kazi ya ukondakta wa mabasi ya abiria, maarufu daladala au matatu, na kwa msaada wa marafiki aliweza kumaliza shule.
Maisha ya kimuziki:
Rekodi Jaguar ya kwanza ilifanyika namo mwaka 2004 na baadae akajiunga na kampuni ya muziki ya Afrika mashariki Ogopa Deejays mnamo mwaka 2005 ambapo na miziki mmoja baada ya mwingine miongoni mwake "kigeugeu." Uliovuma sana na kupokea tuzo nyingi.
Katika kazi yake ya Muziki Jaguar ameweza kupata tuzo mbali mbali.
Tuzo za muziki:
- Mwaka 2011-Tuzo ya muziki wa Afrika mashariki- Mwanamuziki bora wa kiume Afrika mashariki
- Mwaka 2011- Tuzo yaNzumari- Mwanamuziki bora wa kiume Kenya
- Mwaka 2012 -Tuzo ya Kisima-Wimbo bora Kenya
- Mwaka 2012 - Tuzo ya Pearl (Uganda)-Mwanamuziki bora wa kiume
- Mwaka 2012- Tuzo ya muzikila kilimanjaro (Tanzania)-Wimbo bora Afrika Mashariki- Kigeugeu
- Mwaka 2012- Tuzo ya Nzumari-Mwanamuziki bora Afrika Mashariki
- Mwaka 2012-Mshindi wa tuzo ya Channel O- Wimbo bora wa Afrika Mashariki
- Mwaka 2013-Tuzo ya MCSK linalotolewa kwa msanii ambaye nyimbo zake zilichezwa zaidi katika vituo vya redio na kupendwa nchini Kenya.
- Mwaka 2014-Tuzo ya muziki ya Kilimanjaroya Afrika mashariki-Wimbo bora- Kipepeo
- Mwaka 2014- Tuzo ya AFRIMMA (Dallas Texas)-Aliteuliwa kama mwanamuziki bora wa kiume Afrika
Mnamo mwaka 2013 Jaguar alianza kurekodi katika Studio kuu Switch Studios iliyoanzishwa na mmoja wa wazalishaji wa muziki wake wa muda mrefu, Philip Makanda zamani akiwa katika Ogopa Deejays.
Miongoni mwa nyimbo nyingine zilizompatia umaarufu ni Kioo na One centimeter, na kufanya ushirikiano wa kimziki( Kolabo) na wasanii maarufu wa muziki badarani Afrika kama Iyanya kutoka Nigeria, na Mafikizolo kutoka Afrika Kusini katika singo "Going Nowhere"
Siasa
Tarehe 9 Agosti 2017 Jaguar alichaguliwa kuwa Mbunge wa jimbo la Starehe mjini Nairobi kupitia tiketi ya chama tawala cha Jubilee baada ya kuwashinda washindani wenzake Steve Mbogo, Boniface Mwangi na Mwaniki Kwenya.
Jaguar ni kipenzi cha wengi nchini Kenya na ni mwanasiasa ambaye amekuwa na mvuto hasa kwa wafuasi wake ambao wengi wao ni vijana na wanawake.
Mvuto wake umekuwa ukishuhudiwa kila mara anapojitokeza kukutana na wafuasi na wananchi kwa mikutana katika jimbo lake la Starehe ambapo umati mkubwa hujitokeza kumsikiliza na kumshangilia.