Magonjwa ya ngono yaongezeka Uingereza

Idadi ya watu wanaougua magonjwa yanayoambukizwa kwa njia ya ngono inaongezeka nchini Uingereza.

Mnamo mwaka 2018,kulikuwa na watu 447,694 waliobainika kwa mara ya kwanza na maradhi hayo, kiwango hicho kikiwa ni sawa na ongezeko la 5% juu ya idadi ya mwaka 2017 ambapo watu 422,147 ndio waliopatikana na magonjwa hayo kwa mara ya kwanza.

Uhgonjwa kisonono ndio unaoonekana kuwaandama zaidi Waingereza- kwa 26% sawa na wagonjwa 56,259 , idadi hiyo ikiwa ni kubwa zaidi kuwahi kurekodiwa tangu mwaka 1978.

Kulikuwa na visa 7,541 vya kaswende - idadi hiyo ikiwa ni sawa na ongezeko la 5% katika mwaka 2017.

Makundi yaliyomo hatarini zaidi ni vijana pamoja na wanaume wanaofanya ngono na wanaume wenzao.

Magonjwa yatokanayo na ngono (STI's) yanayowakumba zaidi Waingereza ni:

  • Ugonjwa unaosababisha maumivu wakati wa kukojoa au kutokwa usaha katika uume na uke (chlamydia) uliwakumba watu -218,095 , ukichukua 49% ya visa vyote vipya vya magonjwa ya ngono
  • Ugonjwa wa genital warts unaosababisha uvimbe sehemu za siri uliwakumba watu ( 57,318 cases, ukichukua 13% ya magonjwa yanayoambukizwa kwa njia ya ngono
  • Kisonono uliwakumba watu 6,259 sawa na asilimia 13% ya magonjwa yanayoambukizwa kwa ngono
  • genital herpes - maradhi yanayosababishwa na bakteria na kusababisha maambukizi kwenye uke, njia yachoo na kinywani ulichukua 8% ya magonjwa ya zinaa , ukiwa na visa vipya 33,867.

Idadi ya visa vya Kaswende imeongezeka kw amiaka mingi miongoni mwa wanaume na wanawake, licha ya onyo la mara kwa mara kutolewa na madaktari wa umma juu ya hatari za kufanya ngono bila kinga.

Bakteria wa ugonjwa huo husambazwa kutoka mtu mmoja hadi mwingine kupitia ngono bila kinga.

Huenezwi kwa busu, kukumbatia, au viti vya choo au hata kwa kushirikiana taulo au bafu.

Baadhi ya huwa hawana dalili lakini wanaweza kuambukiza wapenzi wao wanapofanya tendo la ngono

Unaweza kutibiwa na dawa za maambukiz (antibiotics), ingawa kumekuwa na ripoti za hivi karibuni zinazosema kuwa imekuwa vigumu kwa baadhi ya watu kutibiwa katika kile wataalamu wanakiita "Super -gonorrhea" ambayo huwa sugu na kushindwa kutibiwa kwa dawa za kawaida.

Watu wenye dalili zozote za kisonono au wanaotokwa na maji maji ya kijani kwenye uke au uume au kusikia maumivu wanapokwenda haja ndogo - wanashauriwa kuwatembelea madaktari bingwa wa uzazi au kliniki ya magonjywa yatokanayo na ngono kwa ajili ya kufanyiwa vipimo.

Ugonjwa wa kisonono husababisha matatizo ya muda mrefu ya kiafya- mkiwemo kushindwa kupata ujauzito miongoni mwa wanawake.

Wataalamu wanahofu uwa watu wengi wanaopata magonjwa haya ya ngono hawapimwi kwa wakati unaofaa.

Wengi wanaaibu kubwa ya kuomba msaada wa matibabu, lakini pia gharama ya matibabu ni tatizo.

Dr Olwen Williams, ambaye ni rais wa shirikisho la huduma za magonjywa ya zinaa na Ukimwi nchini Uingereza anasema kiwango cha mambukizi ya magonjwa yanayosambazwa kwa njia ya ngono kinatisha.

"Miaka ya hivi karibuni tumeshuhudia kwa bahati mbaya kukatwa kwa ufadhili wa huduma za afya ya ngono , na hivyo kukwamisha uwezo wetu wa kukabiliana changamoto katika kipindi hiki kigumu ," alisema.

" Kuendelea kuongezeka kwa magonjwa ya kisonono na kaswende ni jambo linalopaswa kupewa kipaumbele kama dharura ya kiafya ,vinginevyo jambo hili linaweza kusababisha madhara makubwa kwa maisha bora ya watu wengi na mfumo mzima wa afya ."

Wakati huo huo visa vipya vya maambukizi ya ukena uume( genital warts) vinaendela kupungua.

Unawexza pia kutazama: