Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Deni la serikali ya laongezeka huku upinzani ukiitaka serikali ikaguliwe
- Author, Na Dinah Gahamanyi
- Nafasi, BBC Swahili
- Muda wa kusoma: Dakika 2
Waziri wa Fedha na Mipango wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor ametangaza kuwa deni la serikali limeongezeka kwa zaidi ya Trilioni moja.
"Deni la serikali limeongezeka na kufikia Sh.Trillioni 51.03 kutoka shilingi Trilioni 49.86 ya mwaka 2018 ikiwa ni sawa na ongezeko la asilimia 2.35". Alisema leo bungeni.
Awali Mbunge wa Kigoma Mjini (ACT Wazalendo) Zitto Kabwe amesema takwimu zinazotolewa za deni la Taifa si sahihi na kumwomba Spika wa Bunge Job Ndugai kuruhusu ukaguzi maalum wa deni la taifa.
Amesema takwimu zinazotolewa kuhusu deni la taifa si sahihi na akamtaka Spika Ndungai kuunda timu itakayofanya ukaguzi wa deni la taifa.
Akizungumza bungeni leo Bwana Zitto amesema usimamzi wa deni la taifa ni tatizo na kuwataka wabunge kutazama rekodi za Mdhibiti na mkaguzi wa katiibu Mkuu wa hesabu za Serikali(CAG) kwa miaka miwili.
Kwenye ukurasa wake wa Tweeter Bwana Zitto Kabwe ameonyesha namna taarifa kuhusu deni la Tanzania zilivyopotoshwa katika ujumbe wake kwa Ally Saleh:
Mbunge huyo wa upinzani amesema upotoshaji mkubwa wa deni la taifa ni tatizo na akaongeza kuwa mfumo wa malipo na utunzaji wa kumbukumbu za deni la taifa kuusomeki. Amesema Matokeo yake ni kwamba Tanzania ina madeni ambayo hayakurekodiwa na akatoa mfano wa ripoti ya CAG ya mwaka jana ambapo hakukuwa na rekodi ya madeni ya zaidi ya shilingi trilioni 2.
Amesema CAG amekwenda kwa watu waliolikopesha taifa ambao wanasema kuwa kuna pesa ambazo wamezitoa lakini wamesema hawajazipata pesa zao.
Unaweza pia kusikiliza: