Mvua kubwa yaathiri usafiri Dar es Salaam

Mvua kubwa inayoendelea kunyesha katika mji wa Dar es Salaam, Tanzania imeathiri huduma ya usafiri wa umma huku idara ya hali ya hewa ikitoa tahadhari.
Kampuni ya Mabasi ya mwendo kasi (Udart) imelazimika kusitisha huduma zake usafiri kwa mabasi yanayotumia barabara kuu ya Morogoro eneo la Jangwani na barabara ya Kawawa katika Bonde la Mkwajuni kuelekea Morocco.
Taarifa ya Mkuu wa Idara ya Mawasiliano Udart, Deus Bugaywa imeeleza kuwa safari zilizositishwa ni kati ya Kimara -Kivukoni, Kimara - Gerezani, Morocco - Kivukoni na Morocco -Gerezani kuanzia mapema alfajiri ya leo Jumatatu.
"Huduma zinazotolewa sasa ni kati ya Kimara - Mbezi, Kimara -Magomeni Mapipa, Gerezani - Muhimbili, Kivukoni - Muhimbili na Gerezani - Kivukoni" amesema Buyagwa.

Eneo la Jangwani linafahamika kwa kujaa maji mengi barabarani kipindi cha mvua.
Udart wameomba radhi wateja wao na kuongeza kuwa wanaendelea kufuatilia hali ya maji Jangwani na kwamba yakipungua huduma zitaendelea kutolewa.
Baadhi ya watu wamekua wakitoa ushauri kwa wenzao walioshindwa kufika sehemu zao za kazi kutokana na changamoto ya usafiri ya kati kati ya mji kutumia usafiri mbadala.
Wengine waliamua kutumia mtandao wa kijamii wa Twitter kufanya hivyo.
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe, 1
Ukiachana kutatizika kwa usafiri wa mwendokasi, wakaazi wengine wa maeneo mbalimbali ya Dar es Salaam wamekubwa na adha kubwa ya foleni kutokana na mvua hizo kuharibu ama kuziba baadhi ya barabara muhimu.
Mamlaka zaonya mvua kubwa
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (MET) tayari imeshatoa tahadhari juu ya uwepo wa mvua kubwa ambayo itaupiga ukanda wa pwani wa nchi hiyo kwa siku tatu mfululizo kutokea leo Jumatatu Mei 13 mpaka Jumatano Mei 15.
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe, 2
MET wametahadharisha kuwa mvua hizo zitakuwa na madhara makubwa ikiwemo: "Baadhi ya makazikuzungukwa na maji, ucheleweshwaji wa usafiri, kusimama kwa muda kwa baadhi ya shughuli za kijami. Kuanguka kwa kwa majani na matawi ya miti. Kuathirika kwa usafiri wa baharini na uvuvi."
Mamlaka hiyo pia imetahadharisha kuwa kwa siku za Alhamisi na Ijumaa wiki hii, ukanda huo wa pwani ya Tanzania utakabiliwa na upepo mkali.













