Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Mwanamuziki nyota wa Afrika kusini apigwa na mpenzi wake akizungumza na mashabiki kwenye Instagram Live
Raia wa Afrika Kusini wameghadhabishwa na video inayomuonesha mwanamuziki nyota Babes Wodumo, jina halisi Bongekile Simelane akipigwa na mpenzi wake wa kiume Mandla Maphumulo.
Video hiyo iliyowekwa katika mtandao wa kijamii wa Instagram, inamuonyesha mwanamuziki huyo mwenye umri wa miaka 24 akisimama mbele ya kamera, kabla ya mpenzi wake kufika hapo na kuanza kumpiga mara kadhaa kwa kutumia mkono wake.
Babes Wodumo alikuwa chumbani akizungumza na mashabiki wake kwenye Instagram Live
Watu wengi wamemuunga mkono mwanamuziki huyo wa hadhi ya kimataifa kwa kutumia hashtag #StopWomenAbuse.
Waziri wa sanaa na utamaduni Nathi Mthethwa alisema 'amefadhaishwa ' na kile alichokiona.
Aliandika katika mtandao wa twitter - Hatushutumu kitendo hiki cha kidhalimu peke yake, bali tunataka Babes Wodumo kufungua kesi dhidi yake .
Dadake Simela Nonduh aliambia mtandao mmoja wa habari kuwa dada yake 'amefadhaishwa lakini yuko sawa na amepumzika kwa sasa.'
Tayari kesi ya unyanyasaji imefunguliwa katika kituo cha polisi katika mji wa pwani wa Afrika Kusini, Durban na chama cha upinzani cha Economic Freedom Fighters au EFF.
Chama cha upinzani cha Economic Freedom Fighters, EFF ikimesema kuwa mtu yoyote anayeona kufungua kesi hiyo kwa polisi ni kutafuta umaarufu wa kisiasa, hana moyo wa huruma kabisa kwa masaibu yanayowakumba wanawake.