Japan: Kundi kubwa la wanaume waliokuwa nusu uchi waisaka fimbo ya bahati

Chanzo cha picha, Getty Images
Maelfu ya wanaume waliokuwa nusu uchi wanagombania fimbo mbili katika tamasha lililofanyika Japan.
Wanaume elfu kumi waliovalia vinguo vyeupe walishiriki katika sherehe katika nyumba maalum.
Washiriki walipambana kwenye maji ili kutafuta fimbo ambazo zilikuwa zimerushwa katika umati wa watu.
Wale waliopata fimbo zenye urefu wa sentimita 20, zinaitwa"shingi", wanaaminika kuwa ndio wanaume wenye bahati zaidi mwaka huu.

Chanzo cha picha, Getty Images

Chanzo cha picha, Getty Images
Maadhimisho haya yalikuwa ya 510 katika historia ya Japan.
Maelfu ya washiriki hawa uoga maji ya baridi katika mto Yoshii ili waweze kutakaswa kabla hawajaanza kutafuta fimbo ya bahati.
Mara baada ya kumaliza kuoga maji hayo baridi, taa huwasha.

Chanzo cha picha, Getty Images

Chanzo cha picha, Getty Images
Mkuu wa sehemu hiyo ya kuabudia husimama juu kwa mita nne na kurusha fimbo hizo mbili katika mkusanyiko mkubwa wa watu.
Watu wawili watakaoweza kuzipata fimbo hizo hutajwa kuwa washindi wenye bahati.

Chanzo cha picha, Getty Images

Chanzo cha picha, Getty Images
Tamasha la 'Saidaiji-eye' ni miongoni mwa matamasha makubwa katika tamaduni za Japan katika kalenda ya mwaka.
Vilevile tamasha hili linafikiriwa kuwa linaleta mazao mazuri katika mwaka.












