Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Uchaguzi Nigeria 2019: Watu kadhaa wafariki katika mkasa wa mkanyagano Nigeria
Watu kadhaa wameripotiwa kufa na wengine kujeruhiwa baada ya umati wa watu waliofurika katika mkutano wa kampeni za Rais anayetetea kiti chake Muhammadu Buhari kukanyagana.
Tukio hilo lilitokea katika uwanja wa mpira wa mji wa kusini wa Port Harcourt, baada ya umati huo wa watu kusongamana kwa wingi na wengine kuanguka na kukanyagwa katika lango kuu baada ya hotuba ya Rais Buhari.
Siku ya Jumamosi Nigeria itapiga kura kumchagua Rais wa nchi hiyo huku kinyang'anyiro kikali kikitarajiwa kuwa kati ya Rais Muhammadu Buhari na Makamu Rais wa zamani Atiku Aboubakar.
Wengi wa waathiriwa wameripotiwa kuanguka na kukanyagwa na wenzao waliyokuwa wakijaribu kuingia uwanjani kupitia lango lililokuwa limefungwa ili kumfuata Bw. Buhari aliyekuwa ameondoka katika uwanja huo.
Watu waliyoumia wamepelekwa kwa matibabu katika hospitali iliyokaribu.
Ofisi ya rais imesema kuwa rais amearifiwa kuhusu tukio hilo "Tunasikitika kwamba wengi wa wliyofariki ni wafuasi wa chama tawala cha All Progressives Congress (APC)".
Jumla ya vyama 73 vimejiandikisha kugombea katika nafasi ya Urais huku kukiwa na wapiga kura milioni 84.