Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Mwaka mpya 2019: Jeshi la Marekani laomba msamaha kufuatia ujumbe wa bomu
Kitengo cha jeshi la Marekani kinachosimamia silaha za kinyuklia, kimeomba msamaha kwa ujumbe uliotumwa katika mtandao wake wa twitter uliosema kuwa kitengo hicho kilikuwa tayari kuangusha bomu kubwa zaidi ya New York's Times Square ball.
Ujumbe huo uliotumwa mkesha wa kuamkia mwaka mpya uliandamana na kanda ya video inayoonyesha ndege ya kivita aina ya B-2 Bomber ikiangusha silaha.
Kitengo hicho baadaye kilifuta ujumbe huo kikisema kuwa haikuwalengo lao na kuubadilisha na msamaha.
Kisa hicho kilizua hisia kali katika mitandao ya kijamii.
Ujumbe wa twitter wa awali ulisema:
"#tamaduni za TimesSquare# kila mwaka mpya ni kuangusha mpira mkubwa .Iwapo utahitajika, tuko tayari #kuangusha kitu kikubwa zaidi."
Ulichapishwa katika mtandao wa kijamii saa chache kabla ya kuangushwa kwa mpira huo mkubwa juu ya One Times Square, ambalo ni jengo refu la mjini New York, ili kuadhimisha kuanza kwa mwaka mpya.
Utamaduni huo ulianza 1907.
Wakosoaji walishutumu kwa haraka tukio hilo la kitengo hicho cha jeshi.
Aliyekuwa kiongozi wa afisi ya maadili nchini Marekani Walter M Shaub Jr. alituma ujumbe wa twiter akisema: Ni watu gani wanaoendesha taifa hili?
Joe Cirincione , mtayarishaji wa Nuclear Nightmare, kuimarisha usalama duniani alisema: Kwanza sikuamini kwamba hili litafanyika. lakini limefanyika.
''Ni mzaha mbaya wa kitengo cha kusimamia silaha za nyuklia. Ni aibu''.
Kitengo cha kusimamia silaha za kinyuklia nchini Marekani ni mojawapo ya vitengo 10 katika idara ya ulinzi nchini humo.
Makao yake ni kambi ya wanahewa ya Offtutt mjini Nebraska. Kauli mbiu yao ni ''amani ni taaluma' ambayo pia ilitumika katika ujumbe huo uliozua utata.