Nyama choma au chipsi yai? Haya ndiyo madhara ya chakula ukipendacho

Illustration for calculator on environmental impact of different foods

Kupunguza kula nyama na kunywa maziwa ni moja ya njia kubwa ya kupuunguza uchafuzi wako wa mazingira, utafiti mpya wa kisayansi umebaini.

Lakini je kuna tofauti yoyote kimazingira kati ya kula nyama au kuku? Je sahani ya wali inazalisha kwa uchache gesi zinazoongeza joto duniani kuliko sahani ya chipsi?

Na je, mvinyo ni rafiki zaidi wa mazingira kuliko bia?

Ili kujua athari ya kile unachopendelea kula na kunywa kwa hali ya tabia nchi, tumekuandalia kikokotozi ambacho unaweza kujipatia mwenyewe majibu ya maswali ya hapo juu.

Je, wajua chaguo lako la chakula lilivyo na madhara kwa mazingira?

Usilie kwa sababu unashindwa kutumiachati hii
Boresha kirambaza/mtandao wako ili uendelee

Imebuniwa na Prina Shah, na kuendelezwa na Felix Stephenson, Becky Rush.

Presentational grey line

Uchakataji wa chakula unachangia robo ya gesi chafuzi zinazopelekea kuongezeka kwa joto duniani na mabadiliko ya tabia nchi kwa mujibu wa tafiti iliyofanywa na Chuo Kikuu cha Oxford.

Hata hivyo, watafiti waligundua madhara ya vyakula mbali mbali kwa mazingira hutofautiana sana.

Walichogundua watafiti hao ni kuwa, nyama na bidhaa nyengine zitokanazo na wanyama zinachangia zaidi ya nusu ya gesi chafuzi zitokanazo na chakula.

Kati ya vyakula vilivuofanyiwa tafiti, nyama ya ng'ombe na kondoo ndio ambazo zinaathari zaid kwa mazingira.

Presentational grey line
Nyama Choma

Chanzo cha picha, Getty Images

"Vitu tunavyokula vina msukumo mkubwa sana wa hali ya mazingira ya dunia, iwe mabadiliko ya tabia nchi ama ama kupotea kwa uoto wa asili," mtafiti Joseph Poore ameiambia BBC.

Kubadili chaguo lako la vyakula kunaweza kuleta tofauti kubwa ya kimazingira, kuanzia kuhifadhi maji, kupunguza uchafuzi wa hewa na kupotea kwa misitu.

"Mabadiliko hayo yanasaidia kupunguza matumizi ya ardhi kwa asilimia 75, hicho ni kiasi kikubwa sana, hususani ukikipigia hesabu kwa dunia nzima," Dkt Poore ameeleza.

Presentational grey line

Kujua chakula chako kimelimwa na kutayarishwa wapi pia ni jambo la muhimu, sababu chakula cha aina moja kinaweza kuwa na utofauti mkubwa wa uchafuzi wa mazingira kulingana na mahali kilipotokea.

Mathalani, ng'ombe wa nyama aliyefugwa kwenye ardhi ambayo msitu uliteketezwa anachafua mazingira mara 12 zaidi ya ng'ombe ambaye amekuzwa katika mazingira asili.

Ng'ombe wa Amerika Kusini wanachafua mazingira mara tatu zaidi ya wale wa Ulaya na wanatumia ardhi mara 10 zaidi.

chipsi si nzuri pia

Chanzo cha picha, Getty Images

Lakini utofauti hauishii kwenye nyama pekee.

Chokoleti na kahawa zinazozalishwa katika mashamba ambayo misitu minene iliyofyekwa inazalisha gesi chafuzi kwa mazingira mara dufu.

Kwa upande wa nyanya, nzuri zaidi kimazingira ni zile ambazo zilizolimwa nje ama kwenye maturubai ya kisasa yaani greenhouses ambayo ni bora, badala ya yale yanayotumia gesi ama mafuta kujiendesha.

Wanyaji bia ambao wanayapenda mazingira basi wajue kuwa bia zinopakiwa kwenye glasi ama chupa za bati ni mbaya zaidi kwa mazingira.

Presentational grey line

Kikokotozi hiki kimeundwaje?

Dkt Poore kutoka chuo cha Oxford Uingereza na Thomas Nemecek kutoka Zurich waliangalia madhara ya kimazingira ya aina 40 za vyakula ambavyo huliwa kwa wingi duniani.

Utafiti wao ulipitia hatua zote kuanzia kulima, kuchakata, kufungasha na kusafirisha. Utafiti huo haukufikia hatua ya kupika.

Takwimu zilijumuisha mashamba 40,000 na watu 1,600 wanaujihusisha na uchakataji, upakizi na uuzaji wa vyakula hivyo katika maeneo tofauti duniani.