Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Utafiti: Mitetemeko ya Tembo inavyoweza kuashiria walipo
Watafiti wamekuja na njia mpya ya kuwafuatilia tembo, kwa kutumia mitetemeko ambayo wanyama hao huitoa.
Wanasayansi Dkt.Beth Mortimer na Prof.Tarje Nissen Meyer waligundua kuwa tembo huwa wanatengeneza mitetemeko kwa namna ambavyo wanavyotembea kutoka sehemu moja mpaka nyingine.
Njia ambayo wanasayansi wameigundua inaweza kutumika kwa kawaida kupima tetemeko la ardhi pia.
Wataalamu kutoka Oxford aliongelea utafiti huo katika mkutano wa wanawake uliofanyika Califonia.
Walieleza namna ambavyo waliweza kupima mawimbi yanayoweza kusafiri kwa takribani maili nne ardhini.
Walirikodi mitetemeko ambayo yanatolewa na wanyama pori kama Tembo anapotembea au anapoita au kupaza sauti.
Walipiga picha wanyama ili kuhakikisha kuwa mitetemeko hiyo inatoka kwa tembo.
Wanasayansi hao walibaini kuwa sauti nyingine na aina ya udongo huwa inaathiri uwezo wao wa kutoa mitetemeko katika umbali mrefu.
Mitetemeko huwa inasafiri katika michanga kupitia kwenye miamba na vilevile sauti nyingine huwa zinaiingilia.
Kugundua kile ambacho tembo huwa wanakifanya hata kama wako mbali kidogo, kiuhalisia waliona kwamba kunaweza kusaidia kukabiliana na ujagiri.
Utafiti huo ulichapishwa na jarida la sayansi mapema mwaka huu.
Utafiti huu unaweka muongozo mpya wa kujaribu kuelewa mazingira ya tembo na namna wanavyotengeneza mitetemeko hiyo wanayoweza kuitumia wenyewe pia.