Birtukan Mideksa kuiongoza tume ya uchaguzi Ethiopia

Birtukan Mideska had been a harsh critic of the ruling coalition and fled into exile

Chanzo cha picha, ETHIOPIA PM'S OFFICE

Maelezo ya picha, Birtukan Mideska alikuwa mkosoaji mkali wa muungano wa serikali na alikimbilia uhamishoni Marekani

Aliyekuwa jaji na kiongozi wa upinzani nchini Ethiopia ameapishwa kuiongoza tume kuu ya uchaguzi nchini.

Uteuzi wa Birtukan Mideksa ni wa hivi karibuni ulio muhimu wa wanawake waliochaguliwa kufikia sasa kushikilia nyadhifa kuu serikali.

Bi Birtukan alirudi Ethiopia mapema mwezi huu baada ya kuishi uhamishoni kwa miaka 7 Marekani.

Ni miongoni mwa viongozi wa upinzani waliofungwa baada ya uchaguzi uliozusha mzozo mnamo 2005 uliochangia vifo vya mamia ya watu.

Baada ya uteuzi wake, Bi Birtukan amesema anahisi taaluma yake ya u Jaji itamsaidia kutatua mizozo na tofuati ambazo huenda zikazuka katika wadhifa wake mpya.

Lakini ameongeza kuwa Wa Ethiopia kote wamedhihirisha kwamba wapo tayari kwa mageuzi.

Will this Ethiopian girl be able to do things her mother and grandmother couldn't?

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Je matumaini ni yapi kwa wasichana wa Ethiopia kama huyu kuweza kufanya mambo ambayo mamake na nayanake hawakuweza kuyafanya?

"Raia wa Ethiopia wako tayari kujenga mfumo wa demokrasia wanao utaka na kuiwajibisha serikali - na wamelidhihirisha hilo kwa kujitolea ipasavyo ," Birtukan amewaambia waandishi habari.

"Kwahivyo naamini utayari wa umma ni nafasi moja nzuri mno" ameongeza.

Mwandishi wa BBC Emmanuel Igunza aliyepo katika mji mkuu Addis Ababa anasema anakabiliwa na changamoto katika kurudisha imani katika tume ya uchaguzi ambayo mara kwa mara imekabiliwa na shutuma za kuendeshwa na serikali - na atasimamia uchaguzi Mei mwaka 2020.

Kukithiri sura za wanawake katika siasa Ethiopia

Waziri mkuu Abiy Ahmed ametekeleza mageuzi mengi tangu aingie madarakani Aprili.

Taifa la Ethiopia linabadiliika kwa kasi chini ya utawala wake, huku wanawake wakionekana sasa kushikilia nyadhifa kuu za uongozi katika nchi ambayo wanawake wamegubikwa zaidi katika majukumu ya kitamaduni.

Wa Ethiopia hupenda kusema walitawaliwa na Malkia Sheba nyakati za biblia - jambo ambalo wana fahari kubwa nalo, hatahivyo ukweli ni kwamba taifa hilo la upembeni mwa Afrika lina jamii iliyogubikwa kwa mfumo dume.

DATAPIC WOMEN ETHIOPIA

Wanawake ambao ni nusu ya idadi kamili ya milioni 102.5 ya watu nchini, wana majukumu ya kitamaduni zaidi, hususan katika maeneo ya mashambani ambapo muda wao mwingi huwa nyumbani, wakiwatazama watoto, wakitafuta kuni au kuteka maji mitoni na kulima.

Takwimu zilizokusanywa na serikali ya Ethiopia na taasisi nyingine zinaonyesha kuwa:

  • Takriban 25% ya wanawake hutegemea maamuzi ya waume zao.
  • Karibu 50% wamewahi kunyanyaswa katika mahusiano na wapenzi wao.
  • Chini ya 20% ya wasichana wanajiunga na shule za upili.
  • Zaidi ya 40% wanaolewa kabla ya kutimiza miaka 18.

Kwa taswira hii, uamuzi wa Waziri mkuu Abiy Ahmed kuwainua wanawake katika nyadhifa kuu umekaribishwa na wengi, huku makundi ya kutetea haki za binaadamu yakitumai kuwa serikali mpya italiendeleza hili zaidi kwa kuzindua miradi mikubwa katika miezi ijayo kuimarisha maisha ya wanawake wa kawaida.

Abiy, mwenye umri wa miaka 42, amewapa wanawake nusu ya nyadhifa za uwaziri katika serikali - viti 20. Tofauti na viti 4 vilivyoshikiliwa na wanawake katika baraza kubwa zaidi la kiongozi aliyekuwepo Hailemariam Dessalegn.

Chief Justice Meaza Ashenafi's work as a lawyer led to a Hollywood film

Chanzo cha picha, ULLSTEIN BILD

Maelezo ya picha, Jaji mkuu Meaza Ashenafi amesifika kwa harakati zake za kupinga ndoa za wasichana wadogo

Ethiopia na Rwanda ndio sasa mataifa pekee ya Afrika yalio ana idadi sawa ya uwakilishi wa kijinsia katika baraza la mawaziri.

Abiy pia amemteua wakili wa kutetea haki za binaadamu Meaza Ashenafi - ambaye jitihada zake za kukabiliana na ndoa za utotoni ziliigizwa kwenye filamu ya muigizaji mashuhuri wa Hollywood Angelina Jolie mnamo 2014 - kuwa jaji mkuu nchini.

Katika hatua nyingine mbili kuu, mtaalamu wa mawasiliano Billene Aster Seyoum ameteuliwa kuwa msemaji wa rais , huku aliyekuwa afisa wa Umoja wa mataifa Sahle-Work Zewde alichaguliwa katika bunge lililokithiri wanaume kuwa rais wa taifa hilo.

Sahle-Work Zewde is the ceremonial head of state, while Abiy Ahmed (r) holds the political power

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Sahle-Work Zewde ni rais wa Ethiopia, huku Abiy Ahmed (kulia) anashikilia nguvu za kisiasa nchini

Uwepo wa wanawake hawa katika uongozi hivyobasi unamsaidia Abiy - anayetoka katika jamii kubwaa ya Oromo nchini, na ambaye alizaliwa na baba Muislamu na mama Mkristu, kulifikia sio tu suala la usawa wa kijinsia, lakini pia kupanua uungwaji mkono wake miongoni mwa makundi ya wachache na waislamu ambao mara kadhaa hulalamika kutengwa kisiasa.