Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Ninajizuia kuwabusu wasichana kwa sababu ni hatari kwa maisha yangu
Kuna sababu kadhaa zinazoweza kumzuia mtu kubusu - kufa kawaida sio moja ya sababu hizo.
Lakini kwa Oli Weatherall ni kitu cha kumtia wasi wasi mkubwa pamoja na safari za saa nyingi na kula hotelini.
Mwanmume huyo wa miaka 22 kutoka Surrey hukumbwa na madhara mabaya sana mara alapo njugu.
Wakati akiwa mtoto madhara yatokanayo na njugu yalisababisha alazwe hospitalini. Alisema mate yake yaliganda hadi kusababisha asipumue vizuri.
Tangu wakati huo maisha yake yamebadilika kabisa.
Oli anakumbuka wakati wa kwanza alikimbizwa hospitalini baada ya kula mafuta ya njugu kama kisa kibaya zaidi katika maisha yake.
Hakufahamu kile kilikuwa kinaendelea kwenye mwili wake na ngozi yake ilipata madhara mabaya sana.
Sio tu kitu rahisi kujiuzuia kula mafuta ya njugu. Hata kumbusu msichana ni kitu kinaweza kuwa hatari sana kwake.
Kama msichana amekula njugu au amekula chakula kina njugu inawez kuwa hatari.
"Watu washakufa kutokana na hilo," Oli anasema.
"Ni hatari sana ambacho hata watu hawataamini kama hawana madhara kama hayo.
Kula sehemu yoyote isipokuwa nyumbani ni tatizo.
Huku mikahawa ikiwa inahitaji kufahamu kuhusu madhara ya vyakula ni kipi kilicho kwenye chakula chao, Oli anasema mameneja wasio na ujuzia na wahudumu wanaweza kuyafanya maisha kuwa magumu.
Inamaanisha kuwa kila mara akiwa nje kwa saa chache ni lazima apange mlo wake vilivyo.
Maisha yake mengi ni lazima yapangwe kuweza kula kwa njia salama.
Safari za nje ya nchi hazifanyiki kwa sasa pia. Mwanamume huyu anasema kuwa hilo pia linaweza kuwa hatari sana.
Sio tu chakula kwenye ndege. Lakini pia kutoelewa vizuri lugha ya sehemu fulani inaweza kuwa hatari sana kwa maisha.
Mashirika ya ndege yana vifaa vya matibabu na wahaudumu wamepewa mafunzo ya huduma za kwanza lakini Oli ana hofu kuwa hilo halitoshi.