Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Watu 200 wafariki kutokana na Ebola tangu Agosti DRC
Mlipuko wa saa wa Ebola nchini Jamhuri ya Demokrasi ya Congo ndio mbaya zaidi zaidi kuwai kutokea katika historia ya nchi hiyo, kwa mujibu wa wizara ya afya.
Karibu watu 200 wamefariki dunia tangu Agosti, kwa mujibu wa maafisa, huku zaidi ya 300 wakithibitishwa kuambukizwa ugonjwa huo.
Congo imekumbwa na misukosuko ya miaka mingi na jitihada za kukukabiliana ugonjwa huo zimetatizwa na mashambulizi dhidi ya watoa huduma za afya.
Wakati huu visa 319 vimeandikishwa na pia vifo 198, waziri wa afya Oly Ilunga alisema.
Karibu nusu ya waaathiriwa ni kutoka mji wa Beni, mji wenye wakaazi 800,000 eneo la Kivu Kaskazini, kwa mujibu wa halmashauri ya kitaifa ya afya.
Mlipuko wa sasa ndio wa kumi kuikumba Congo na mbaya zaidi tangu ule wa kwanza wa mwaka 1976.
Mlipuko wa mwaka 1976 kwa kile kilikuwa ugonjwa usiojulikana ulizua wasi wasi mkubwa lakini ulidhibitiwa na wataalamu walioutambua kwa haraka.
Ebola husambaaa kupitia maji maji ya mwila na mara nyingi huwa hatari sana kwa maisha