Papa Francis kualikwa Korea Kaskazini na Kim Jong-un

Chanzo cha picha, Getty Images
Ofisi ya rais wa Korea kusini imetangaza kuwa kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un amemualika papa Francis kutembelea nchi hiyo.
Mualiko huo wa Pyongyang utawasilishwa na rais wa Korea kusini Moon Jae-in ambaye anatarajiwa kuwa Vatican wiki ijayo akiwa katika ziara zake barani ulaya.
Inaelezwa kuwa Papa Francis sio papa wa kwanza kualikwa kutembelea Korea kaskazini ,ingawa papa John Paul wa pili aliwahi kualikwa pia.
Korea kaskazini na Vatican hawana uhusiano wowote wa kidiplomasia.
"Katika kikao na papa,Moon anategemea ujumbe kutoka kwa mwenyekiti ambaye ni Kim Jong-un ambaye anamkaribisha Papa kwa moyo mmoja kutembelea mji mkuu wa korea kaskazini Pyongyang", Msemaji wa Moon , Kim Eui-kyeom amewaambia waandishi.
Mualiko huo utakuwa ni hatua ya hivi karibuni ya makubaliano kutoka Korea kaskazini.

Chanzo cha picha, Reuters
Mara ya kwanza Kim alifanya mkutano na rais wa Marekani Donald Trump mwanzoni mwa mwaka huu na mikutano mingine mitatu ya wakorea ilifanyika.
Mwaka 2000,baba yake Kim Jong-un alimualika Papa John Paul ii kutembelea Korea kaskazini baada ya papa kunukuliwa kudai kuwa itakwa maajabu kama atakwenda huko.
Hata hivyo mualiko huo na rais wa Korea kusini Kim Dae-jung haukuwahi kufanyika.
Kwa mujibu wa vyombo vya habari ,ulisema Vatcan ilisisitiza muda ambao papa anaweza kutembelea ni kama mapadre wa katoliki watakubalika korea kaskazini.
Je,kuna uhuru wa diniKorea kaskazini
Katiba ya Korea kaskazini ilihaidi kuwa kutakuwa na haki ya kuabudu na taifa halitaingilia miongozo iliyowekwa na makanisa.
Lakini kiuhalisia hakuna uhuru wa dini,alisema Arnold Fang mtafiti kutoka Amnesty International.
Ripoti ya umoja wa mataifa ya mwaka 2014 ilibanisha kuwa wakristo katika eneo hilo huwa wananyanyaswa na kupata adhabu pale wanapoonyesha imani yao hadharani.
Kwa mujibu wa kituo cha habari cha NK kimesema, kanisa katoliki litaendelea kuepo Korea Kaskazini ingawa nchi hiyo haina uhusiano rasmi na Vatcan.
Mamlaka inayoongoza jumuiya ya kikatoliki pia inajumuishwa kutokuwa na uhusiano na Vatcan .
Kwa mujibu wa AFP na KCA ,wakatoliki wanakadiriwa kuwa 3000 nchi nzima wakati Umoja wa kimataifa inawanawakadiria wakatoliki kuwa 800.
Korea kaskazini haijaweka wazi kuhusu ziara ya wamisionari wageni.
Kenneth Bae ni mchungaji kutoka Marekani ambaye aliongoza ziara ya kikristo Korea kaskazini na kufungwa miaka 15 pamoja na kupewa kazi ngumu mwaka 2013 na aliachiwa huru mwaka 2014 baada ya kuwa na matatizo ya kiafya.












