Tetesi za Soka Ulaya Jumapili 07.10.2018: Zidane, Mourinho, Pogba, Ndombele, Henry, Dembele, Ibrahimovic

Wakuu wa Manchester United wamemshauri Zinedine Zidane kutotafuta umeneja kwingine wakati wakiamua hatma yake Jose Mourinho. (Mirror)

Mashabiki wa United walipigwa picha na sanamu ya meneja wa zamani wa Real Madrid Zinedine Zinade, 46 nje ya Old Trafford kabla ya ushindi wa siku ya Jumamosi dhidi ya Newcastle. (Eurosport)

Machester United watahitajika kumlipa Mourinho pauni milioni 29 ikiwa watamfuta meneja huyo mwenye maiaka 29 lakini kiwango hicho kitashuka hadi pauni milioni 10 ikiwa atamaliza msimu na United washindwe kumaliza katika nafasi za Ligi ya Mabingwa. (Mirror)

Mourinho alifichua kuwa alipokea ujumbe wa imani naye kutoka bodi ya Manchester United kabla ya ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Newcastle. (Times)

Manchester City watahitaji kuvunja rekodi yao ya kusaini wachezaji kumsaini kiungo wa kati wa Lyon Tanguy Ndombele baada ya klabu hiyo ya ufaransa kumwekea thamani ya pauni milion 70 mchezaji huyo wa miaka 21 mwezi Januari. (Star)

Manchester United wamemuambia Paul Pogba kuwa hatauzwa mwezi Januari licha ya mfaransa huyo wa miaka 25 kuripotiwa kuwa na nia ya kujiunga na Barcelona baada ya wao kuonyeha nia ya kumsaini. (Mail)

Straika za zamani wa Arsenal Thierry Henry ameibuka kuwa bora kuchukua umeneja huko Aston Villa baada ya mazungumzo na wakuu wa klabu hiyo. (Sunday Telegraph)

Meneja wa Celtic Brendan Rodgers anafikiriwa kuwa na nia ya kujiunga na Villa. (Star)

Kiungo wa kati wa Tottenham Mousa Dembele, 31, hatarajiwi kujadili mkataba mpya na huenda akaondoka wakamti mkataba wake utakwisha mismu wa joto akitarajia kuhamia China au mashariki ya Kati. (Sun)

Mshambuliaji wa zamani wa Manchester United Zlatan Ibrahimovic, 37, ambaye sasa anaichezea LA Galaxy yuko tayari kuzungumza na AC Milan kuhusu kurejea kwake kwa mujibu wa ajenti wake Mino Raiola. (Sun)

Arsenal wanatarajiwa kumwendea nahodha wa Porto Hector Herrera, 28, kama atayechukua mahala pake Aaron Ramsey, 27, ambaye anatarajiwa kuondoka Emirates mwezi Januari au msimi ujao wa joto. (A Bola, via Football London)

Meneja wa Wolves Nuno Espirito Santo anasema kuna mengi yatatoka kwake baada ya kupanda hadi nafasi ya saba katika Ligi ya Premier kupitia ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Crystal Palace, na kuendelea na rekodi yao ya kutoshindwa hadi mechi sita. (Express and Star)

Bora Kutoka Jumapili

Habari za ndani toka Machester United zinasema kocha Jose Mourinho atatimuliwa kazi kwenye mapumziko haya ya mwishoni mwa juma kama timu yake itapata matokeo mabaya dhidi ya Newcastle United ( Daily Mirror)

Mshambuliaji nyota wa klabu ya Paris St-Germain na timu ya taifa ya Brazil Neymar amefanya mazungumzo na kiungo wa Manchester United Paul Pogba kumshawishi kujiunga na mabingwa hao wa League 1 baada ya kutokua na mustakabali mzuri wa baadae kwa kiungo huyu mwenye miaka 25. (Goal)

Kocha wa Crystal Palace Roy Hodgson amesema timu yake inaweza kumsajili kiungo wa Chelsea Roben Loftus-Cheek,ambaye alicheza kwa mkopo kwenye timu hiyo msimu uliopita (Talksport)

Timu ya Arsenal itamsajili kiungo raia wa Paraguay mwenye umri wa miaka 24 anaichezea timu ya Atlanta United Miguel Almiron,Hayo yamesema na Rais wa timu hiyo ya Marekani Darren Eales (Fox Deportes USA, in Spain)