Iran yailaumu Marekani baada ya wanajeshi wake na raia 25 kuuawa huko Ahvaz

Chanzo cha picha, EPA
Rais wa Iran Hassan Rouhani ameilaumu Marekani kufuatia shambulizi baya lililolenga gwaridi ya jeshi.
Watu wenye silaha waliwafyatulia risasi wanajeshi wa Iran kwenye mji ulio kusini magharibi wa Ahvaz siku ya Jumamosi kwenye shambulizi lilalodaiwa na kundi linaloipinga serikali na wanamgambo wa Islamic
Rouhani alisema Marekani na mataifa ya Ghuba yaliunga mkono shambulizi hilo.
Bw Rouhani atakutana na Trump wakati wa mkutano wa Umoja wa Mataifa wiki hii.

Chanzo cha picha, AFP
Shambulizi hilo la Jumatatu liliwaua watu 25 wakiwemo wanajeshi 12, raia waliokuwa wakitazama gwaride na msichana wa umri wa miaka minne.
Ahvaz National Resistance, sehemu ya kundi lilinalodai kupigania haki za Waarabu wacache kwenye mko wa Khuzestan nchini Iran, lilisema kuwa ndilo lilifanya shamblizi hilo huku nayo IS ikidai kuhusika.
Hakuna kundi lililodai lilionyesha ushahidoi wa kuhusika.
Kwa nini Iran inalaumu nchi za Ghuba?
Iran awali imedai kuwa wafuasi wa Saudi Arabia inayaunga mkono makundi yaliyojitenga nchini Iran.
Nchi hizo zote mbili zimekuwa ziking'ang'ania kuidhibiti kanda hiyo kwa miongo kadhaa na zinashirikiana kwenye vita eneo hilo zikiunga mkono makundi hasimu nchini Yemen na Syria.

Chanzo cha picha, Getty Images
Uhasama huo wa miongo kadhaa unachochewa na tofauti za kidini wakati - Iran ina Washia wengi huku Saudi Arabia ikijitambua kama taifa kuu la dhehebu la Sunni.
UAE na Bahrain ni washirika wa karibu na Saudi Arabia.
Iran pia ilidai kuwa washambualiaji walikuwa na uhusiano na hasimu wake mkuu Israel.
Kwa nini kuna uhusiano mbaya kati ya Marekani na Iran?
Pande hizo mbili zimekuwa na uhusiano mbaya kwa miongo kadhaa.
Marekani inailaumu kwa kundesha programu ya silaha za nyuklia, madai ambayo Iran inayakana.
Mwaka 2015 chini ya uongozi wake Barack Obama, Marekani na Iran waliafikia makubaliano ya nyuklia ambayo pia yalitiwa sahihi na China, Urusi, Uingereza, Ufaransa na Ujerumani ambapo Iran ilipunguza shughuli zake za nyuklia ili ipate kuondolewa vikwazo.
Hata hivyo uhusiano huo ulidorora zaidi bada ya Trump kuingia madarakani na kuiondoa Marekani kutoka kwa mkataba huo.












