Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Koffi Annan kuzikwa Ghana, Alhamisi
Mwili wa aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Kofi Annan, ambaye alifariki mwezi uliopita, umewasili katika nchi aliyozaliwa, Ghana.
Mwili wake uliwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kotoka International Airport mjini Accra, ukisindikizwa na familia yake na maafisa wengine wa Umoja wa Mataifa.
Anatarajiwa kuzikwa kitaifa siku ya Alhamisi.
Kulikuwa na hali ya maombolezowakati mwili wake ukiwasili uwanjani hapo na kupokelewa na Rais wa Ghana Akufo Addo na viongozi wa kimila na kwa heshima ya kijeshi.
Mwili wake umehifadhiwa katika Ukumbi wa Kimataifa wa mikutano wa Ghana, wakati ukisubiri kuzikwa.
Kofi Annan alikuwa ni Katibu mkuu wa kwanza wa Umoja wa Mataifa, kutoka katika eneo la kusini mwa jangwa la Sahara na kuleta mafanikio sio tu katika bara la Afrika, lakini pia dunia nzima.
Aliwahamasisha vijana wengi nchini mwake na waliheshimu kile alichosimamia.