Aretha Franklin 'malkia wa muziki wa soul' afariki dunia

Chanzo cha picha, GETTY IMAGES
Aretha Franklin ni malkia wa muziki wa taratibu 'queen of soul' na alikuwa mwanamke wa kwanza kuchaguliwa katika Rock na Hall of Fame amefariki dunia huko Detroit akiwa na umri wa miaka 76.
Mwanamuziki huyo alikuwa anasumbuliwa na ugonjwa wa saratani tangu mwaka 2010 na alitangazwa kuwa anaumwa hapo mwaka jana wakati akistaafu katika muziki.
Muziki wake ambao ulijulikana zaidi ulikuwa ni 'Respect and Think' ambao ulikuwa katika nyimbo 20 bora zilizopendwa zaidi nchini Marekani kwa miongo saba.

Chanzo cha picha, GETTY IMAGES
Aretha aliweza onyesho lake la mwisho mwezi novemba katika gala iliyoko mjini New York akiwa amesaidiwa na taasisi ya Elton John ' Elton John Aids Foundation'
Aretha alizaliwa Memphis na alianza kuimba kama muimbaji wa dini na mpiga kinanda na alikuwa muhubiri katika sherehe za ubatizo.
Franklin alianza kufundishwa katika umri mdogo kuwa nyota wa mziki wa dini kama ilivyokuwa kwa Mahalia Jackson na Clara Ward.

Chanzo cha picha, Getty Images
Franklin aliweza kuhangaika kupata umaarufu katika umri mdogo akiwa chini ya rekodi za Columbia ambazo zilijitahidi kuondoa aibu aliyokuwa nayo na kuiweka sauti yake inayovutia kuweza kung'ara duniani.
Mwanamuziki Elton Jon ameandika salamu zake za pole katika ukurasa wa insagram na kusema kifo cha Aretha Franklin kimeshtua kila mmoja anayependa muziki wa kweli.

Chanzo cha picha, Getty Images
Muziki kutoka moyoni ,kwenye nafsi na kanisani.
"Sauti yake ilikuwa ya kipekee,jinsi alivyokuwa anapiga piano kwa ufanisi...nilimpenda na nilithamini talanta yake .Mungu ambariki na salamu zangu za pole kwa familia"Elton.













