Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Je ni kweli Al shabaab ina mfumo bora wa kutoza kodi?
Taasisi moja ya utafiti nchini Somalia imesema kwamba kundi la wapiganaji wenye itikadi kali la Al Shabaab lina mfumo bora wa ulipaji kodi ambao unasababisha kupata mamilioni ya dola kwa mwaka.
Kundi hilo la Alshabaab limekuwa likifanya mashambulizi ya kigaidi na maelfu ya watu kupoteza maisha, na kusababisha uchumi wa Somalia kuzorota, hali ambayo pia imeifanya nchi hiyo kuzalisha wakimbizi maeneo mbalimbali duniani.
Taasisi hiyo ya Hiraal imesema ingawa kundi hilo lenye itikadi kali linafanya shughuli zake tu katika maeneo ya kusini mwa Somalia, hulazimisha watu katika maeneo mengi ya nchi kulipa kodi, ikiwemo katika mji mkuu Mogadishu, ambao unashikiliwa na majeshi ya serikali.
Mkuu wa taasisi ya Hiraal Hussein Sheikh- Ali amesema kwamba wapiganaji hao wenye itikadi kali wamejipatia zaida ya dola za Kimarekani milioni 10 katika kipindi cha mwaka 2016 kutokana na kodi iliyotokana na mifugo.
''Al Shabaab kama kundi lingine la wapiganaji na la kigaidi limekuwa likikusanya fedha kutoka vyanzo mbalimbali vya mapato. Lilianza kwa kukusanya mapato kidogo kutoka kwa watu waliokuwa wakiwaunga mkono ndani na nje ya nchi.
''Lakini kundi hilo lilipopanuka na kuwa kubwa walianza kujenga mfumo wao wa ukusanyaji ushuru katika maeneo yote ya Somalia'' anasema Hussein Sheikh-Ali.
Mfumo wa kodi
Al-Shabab linaonekana kuwa na mfumo unaofanya kazi vizuri wa utozaji kodi ambao wachache wanasubutu kuukiuka, kwa mujibu wa gazeti la Marekani Washington Post.
Hili linatajwa kuleta mtiririko wa kipato cha kuimarika.
Na zaidi, al-Shabab linaonekana kuwa na kiwango kidogo cha rushwa tofauti na baadhi ya mataifa katika nchi zinzaoendelea.
Pengine hilo ndilo linaloonekana kuufanya mfumo wa kundi hilo kuwa bora.
Taasisi ya Hiraal imesema kwamba wakati baaadhi ya watu na biashara hulipa kwa fedha taslimu, wapiganaji hao wana uwezo wa kupata kiasi cha dola milioni 10 kwa mwaka kutoka kwa watu ambao wanalipa kupitia mifugo yao.
Mwaka jana serikali ya Somali kwa mara ya kwanza iliwaonya wafanya biashara dhidi ya kulipa kodi kwa Al Shabaab baada ya kuibuka taarifa kuuhusu utozaji huo.
Waziri wa ulinzi Somalia, Mohamed Abukar Dualle aliwaambia waandishi habari,
"Utawawajibisha na kuzifunga biashara za watu wanaolipa kodi kwa al Shabaab. Serikali haitokubali ufadhili kwa kundi hilo," waziri alisema.
Idara hiyo ya ulinzi ilionya kuwa hatua za kisheria zitaidhinishwa dhidi ya watakokiuka maagizo hayo ya serikali.
Na onyo hilo lilitolewa katika wakati ambapo kundi wapiganaji hao wa kiislamu wal;ikuwa wamepiga marufuku matumizi ya shilingi ya Somalia katika maenoe ya kati na ya kusini wanayoyadhibiti kutokana na kiolichotajwa kuwa ongezeko la fedha bandia.
Biashara zilisita katika enoe la Hiiraan kufuatia marufuku dhidi ya sarafu hiyo ya pekee inayotumika nchini Somalia.
Al Shabaab imetekeleza mashambulio yaliosababisha maafa makubwa licha ya kupoteza sehemu kubwa ya udhibiti wake kutokana na operesheni ya vikosi vya Umoja wa Afrika AMISOM vinavyolinda amani Somalia.
Kundi hilo limekuwa likidai kuwa linataka kuwatimua walinda amani hao, kuipindua serikali ya Somalia inayoungwa mkono na mataifa ya magharibi na kuidhinisha sheria za dini ya kiislamu Somalia.