Nilikuwa na uraibu wa kumeza vidonge 57 kwa siku

Disemba mwaka 2017 mwanamke Muingereza Laura Plummer alifungwa jela kwa miaka mitata kwa kupeleka vidonge 300 vya kupunguza maumivu vya Tramadol nchini Misri.
Licha ya hukumu hiyo kuwashanza za wengi chini Uingereza kisa hicho kiliweka waza tatizo la uraibu wa dawa hizo unaowakumba mamilioni ya watu nchini Misri.
"Wakati ni nikiwa na umri wa miaka 15 nikicheza mchezo kwenye duka la mtandao, mtu alinichoza. Nilichukua kifaa nikamgonga kichwani, nilikuwa kipiga kelele na kumtukana kila mtu, na hata nilivunja madirisha."
Abdul Hameed sasa akiwa na miak 24 anakumbuka wakati alikuja kufahamu kuwa uraibu wake wa dawa hiyo ulikuwa umevuka mpaka.
Kama vijana wengi nchini Misri alianza kwa kutumia robo ya miligramu 100 ya dawa hiyo.

Chanzo cha picha, Ahmed Maher
"Nilihisi kuwa nilikuwa bingwa," anasema. "Ningefanya chochote."
Ilifika hadi wakati Abdul Hameed alikuwa akimeza vidonge 57 kwa siku na mara nyingi nusura afe.
Ukweli
Kulingana na mfuko wa kutibu watu walio na uraibu, mtu mmoja kati ya watu watatu nchini Misri wakiwa hao ni karibu watu milioni 30, wana uraibu wa dawa za kupunguza maumivu na dawa wanayotumia zaidi ni Tranadol.
Kwanza dawa hii ilionekana kwenye masoko ya Misri miaka 20 iliyopita. Ni nafuu kuliko heroin na inapatikana kwa njia rahisi pia. Ilipata umaarufu kwa waraibu na kusambaa kwa haraka kwa watu wengine kama njia ya kupunguza maumivu na misongo mingine katika maisha.
Tramadol imekita mizizi nchini Misri na hadi mashirika ya kuwasaidia walio na uraibu yanasema kuwa yanapokea zaidi ya simu 500 kwa siku kutoka kwa watu wanaotaka kuachana na uraibu huo.
Waraibu mara nyingi huwa ni vijana.

Chanzo cha picha, PA












