Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Watu 30 walazwa hospitalini Mombasa kutokana na ugonjwa wa chikungunya
Watu 30 wamelazwa kwenye hospitali mbali mbali za kaunti ya Mombasa pwani mwa Kenya baada ya kuugua ugonjwa wa Chikungunya, kwa mujibu wa shirika la habari la serikali KBC.
Gavana wa Mombasa Hassan Joho, amezindua magari matano yenye mashine na dawa kunyunyiziwa katika kaunti hiyo wakati ugonjwa unazidi kuwatishia watu zaidi.
Chini ya miezi mitatu iliyopita kaunti ya Mombasa ilikuwa ikikabiliana na mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu ambapo watu kadhaa walilazwa hospitalini na maeneo kadhaa ya mankuli kufungwa katika kaunti hiyo.
Joho alithibitisha kuwa kumekuwa na visa 120 vya wagonjwa huo na visa 32 vilivyothibitiwa kati ya hivyo vimedai kuwa vile vya ugonjwa wa chikungunya.
Kufuatia ugonjwa huo kusambazwa na mbu Gavana Joho amewashauri wenyeji wa Mombasa kushirikiana kwa karibu na serikali ya kaunti kuondoa mazingira salama kwa mbu.