Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Chupa ya mvinyo ghali zaidi duniani yaibwa Denmark
Polisi nchini Denmark wanachunguza kisa cha wizi wa chupa ya mvinyo inayodaiwa kwa ghali zaidi duniani ya thamani ya dola milioni 1.3.
Chupa hiyo iliyotengenezwa kutoka kwa dhahabu na fedha na kifuniko cha almasi ilikopeshwa baa moja huko Copenhagen ambayo ilikuwa imekusanya chupa za mvinyo kwa maonyesho.
Mmiliki wa baa hiyo Brian Ingberg alisema chupa ilikuwa imetumiwa kwenye kipindi kinachofahamika kama House of Cards.
Picha za CCTV zinaonya mvamizi akishika chupa hiyo na kutoroka.
Polisi wanasema kuwa haijuikani ikiwa mwzi huyo ambaye alivamia siku ya Jumanne alivunja au alikuwa na ufunguo.
Bw. Ingberg ambaye ni mmliki wa bar aliiambia runinga ya TV2 kuwa alikuwa ameikopa chupa hiyo kutoka kwa kampuni moja huyo Latvia.