Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Vikwazo: Raia wa Korea Kaskazini wanaofanya kazi ugenini kurudi kwao
Rais DonaldTrump wa Marekani, amelipongeza baraza kuu la usalama la Umoja wa Mataifa kwa kuidhinisha vikwazo vipya dhidi ya Korea Kaskazini.
Bwana Trump ameandika katika mtandao wake wa Twitter, kwamba hatua hiyo ni ishara wazi kwamba ulimwengu unataka amani na wala sio mauti.
Vikwazo hivyo vilivyowasilishwa na Marekani vinaungwa mkono na China ambaye ni mshirika mkuu wa Korea Kusini.
Kufuatia vikwazo hivi vipya uagizaji mafuta wa Pyongyang utapunguzwa hadi asilimia tisaini, huku raia wa Korea Kaskazini wanaofanya kazi katika mataifa ya kigeni wakitakiwa kurudi makwao.
Wizara ya mambo ya nje ya Uchina imesema vikwazo hivyo havitarajiwi kuwa na athari kubwa za kibinadamu.
Hata hivyo imetowa wito kwa pande zote kushauriana ili kujaribu kupunguza taharuki katika rasi ya Korea.