Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Kansela Merkel awekwa njia panda
Mazungumzo kuunda serikali ya mseto nchini Ujerumani yamevunjika, hali ambayo inaweka njia panda mstakabali wa Kansela Angela Merkel.
Baada ya wiki nane ya majadiliano chama chenye mrengo wa kati cha Centrist Free Democrats -FDP- kimejitoa kikilalamikia tofauti zisizoweza kusuluhishwa na chama cha Merkel cha Christian Democrats na vyama vingine katika mazungumzo.
Baadaye leo bibi Merkel atakutana na Rais wa Ujerumani Frank-Walter Steinmeier, ambaye ndiye mwenye nguvu kuitisha uchaguzi mpya.
Bibi Merkel ameonya kuwepo kwa magumu katika wiki zijazo.
Kiuhalisia makubaliano9 ya muungano huo yanawezekana lakini bado haijawa wazi iwapo kuna uwezekano wowote washiriki kufanya umuhimu wa kupata suluhu.