Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Manowari nyingine ya jeshi la Marekani yagongwa baharini
Meli ya jeshi la Marekani ilikumbwa na uharibfui kidogo baada ya kugongana na chombo kingini cha Japan pwani ya Japan.
Chombo hicho cha kibiashara kilikosa mwelekeo na kuigonga manowari hiyo ya Marekani ya USS Benfold eneo la Sagami Bay.
Hakuna mtu aliyejeruhiwa kwenyo vyombo hivyo viwili, jeshi la Marekani lilisema na kuongeza kuwa uchunguzi unafanyika.
Hiki ndicho kisa cha hivi punde kinachoikumba Meli ya jeshi la Marekani miezi ya hivi karibuni.
Katika taarifa jeshi la majini la Marekani lilisema kuwa manowari hiyo ilikumbwa na uharibifu kidogo,
Mwezi Agosti wanajeshi 10 wa Marekani waliuwa wakati Manowari ya USS John S McCain, iligongana na meli ya kubeba maftua nchini Singapore.
Mwezi Junuari wanajeshi 7 wa Marekani waliuawa wakati Manowari ya Marekani ya USS Fitzgerald, iligongana na meli ya mizigo kwenye maji ya Japan karibu na bandari ya Yokosuka.