Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Chui milia mla watu kuuliwa kwa kupigwa risasi India
Mahakama katika jimbo la magharibi mwa India la Maharashtra, imedumisha amri ya kuuliwa kwa chui milia wa umri wa miaka miwili ambaye amewaua watu 4.
Wanaharakati wa wanyamapori wamepinga agizo ya kuuliwa chui huyo kwa kupigwa risasi, iliyotolewa na idara ta misitu tarehe 23 mwezi Juni.
Chui milia huyo alikamatwa mara ya kwanza mwezi Julai baada ya kuua watu 2 na kuwajeruhi wengine 4 katika mji wa Brahmapuri huko Maharashtra.
Aliachiliwa huru katika makao ya kuwatunza chui milia lakini tangu wakati huo amewaua watu wawili zaidi
Wanaharakati wa wanyamapoti wanasisitiza kwa chui anastahili kudungwa dawa ya kulala na kuhamishwa kwenda eneo lingine.
Maafisa ambao wamekuwa wakimfuatilia mnyama huyo kwa jina Kala, wanasema kuwa ametembea zaidi ya kilomita 500 tangu aingine hifadhi tarehe 29 Julai.
India ni nyumbani kwa asilimia 60 ya chui milia duniani waliohatarishwa na watu wanaowaua kwa sehemu za mwili zinazotumiwa kwa madawa ya kitamaduni nchini China.
Vifo vya chui milia vimeongezeka hivi karibuni. Mwaka 2015 maafisa nchini India waliripoti kuuliwa kwa chui milia 80 ikilinganishwa na 78 mwaka uliotanguliwa.