Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
China yaiwekea vikwazo Korea Kaskazini
Uchina imeimarisha vikwazo dhidi ya Korea Kaskazini, ambapo imetangaza usitishaji wa ununuzi wa nguo kutoka Korea kaskazini mbali na uuzaji wa mafuta kwa taifa hilo kuanzia leo na baada ya muda fulani.
Hatua hiyo inaambatana na maagizo ya vikwazo yaliyowekwa na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa siku 11 zilizopita.
Wachanganuzi wanasema kuwa vikwazo hivyo vitaathiri sana raia wa Korea Kaskazini iwapo vitatekelezwa kwenye mpaka kati ya mataifa hayo ambao hauna doria ya kutosha.
Utengenezaji wa nguo ni huduma muhimu ya pili inayoletea Korea Kaskazini fedha za kigeni na sehemu nne kwa tano ya nguo hizo hupelekwa Uchina.
Inakisiwa kuwa zaidi ya watu 100,000 wanafanya kazi katika sekta hiyo nchini Korea Kaskazini.