Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Idadi ya wanaohama Korea Kaskazini wakienda Korea Kusini yapungua
Korea Kusini inasema kuwa idadi ya watu walio ihama Korea Kaskanizi imepungua kwa zaidi ya asilimia 10 mwaka huu.
Shirika la habari la serikali lilisema kuwa wizara ya kuwainganisha watu ya Korea Kusini, ilirekodi jumla ya watu 780 raia wa Korea Kakskazini waliowasili kati ya mwezi Januari na Agosti mwaka huu.
Korea Kaskania na China wanaaminiwa kuongeza ulinzi zaidi katika mpaka na kufanya vigumu kwa wale wanaohama kuvuka mpaka.
Zaidi ya nusu kati ya wale waliohama Korea Kaskazini mwaka huu ni wakulima, wafanyakazi wanaoaminiwa kukimbia umaskini huku asilimia tatu wakiwa ni wanajeshi na maajenti wa serikali.